Antonio
Conte amekanusha kuwa Juventus iko kwenye mpango wa kumchukua Didier Drogba kuelekea
Turin lakini amesema Fernando Llorente yuko katika mipango ya mapendekezo.
Didier
Drogba kwasasa anasaka klabu ya kuelekea kutoka katika klabu yake ya sasa Shanghai
Shenhua ya dirisha dogo la usajili.
Juve maarufu
kama Bianconeri tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa majira ya baridi, imekamilisha
usajili wa mchezaji mmoja tu mlinzi Federico Peluso aliyetokea Atalanta lakini
pia wakiwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Drogba, amekuwa
akihusishwa na Juve katika kipindi cha hivi karibu wakati ambapo Athletic
Bilbao ikiweka wazi kuwa mshambuliaji wao Llorente ameanza mazungumzo ya
kujiunga na Juventus mara baadya mkataba wake kumalizika.
Mancini: klabu iliguswa na mzozo
wangu na Balotelli lakini wananiunga mkono.
Roberto
Mancini amesisitiza kuwa mmiliki wa klabu na mwenyekiti wa klabu ya
Manchester United wameonekana kuridhishwa na hatua yake ya kutaka kumrekebisha kumpa nafasi
zaidi Mario Balotelli.
Mancini amesema
hapingani na hali ya sintofahamu iliyojitokeza wakati wa mzozo wake na Balotelli
katika uwanja wa mazoezi ambapo meneja huyo wa City alionekana kwenye picha
akimkunja mshambuliaji wake kijezi cha juu cha mazoezi(bips).
Mtaliano
huyo amesema mmiliki wa klabu Sheikh Mansour na mwenyekiti wa klabu Khaldoon al
Mubarak wamekubaliana na mawazo yake ya kutaka kumpa muda zaidi wa
kujirekebisha sambamba kumpa fursa nyingine.
Amenukuliwa Mancini
akisema,
"kwakweli
wananipa sapoti mimi na timu kwa ujumla na nadhani wananipenda na wana matumaini
kuwa Mario anaweza kubadilika na tufikirie zaidi juu ya kazi yake na mpira"
Boateng huenda akaondoka Italia.
Kiungo wa AC
Milan Kevin-Prince Boateng anatarajiwa kutoa maamuzi yake magumu katika siku zijazo
kama ataendelea kucheza soka katika ligi kuu ya nchini Italia Serie A au kuondoka,
kufuatia kitendo cha kibaguzi alicho fanyiwa wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi
ya Pro Patria mwishoni mwa juma.
Nyota huyo
wa kimataifa wa Ghana Boateng pamoja na wachezaji wenzake wa Milan waliamua
kuondoka uwanjani kufuatia kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki.
Shirikisho la
soka la Italia (FIGC) limesema litaendesha uchunguzi, wakati ambapo kitendo cha
kususia kuendelea na mchezo huo kuonekana kuwavutia watu wengi mashuhuri
akiwemo kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli.
Boateng
ambaye ana mkataba mpaka 2014, anafikiria kuondoka nchini Italia.
Amenukuliwa na
gazeti la Bild la nchini Italia Bouteng mchezaji huyo mzaliwa wa Ujerumani akisema
"hili si
jambo la mzaha, nipe siku tatu nilale niamke na nikutane na wakala wangu Roger
Wittmann wiki ijayo tuone kama kama kuna haja ya kuendelea kucheza Italia"
No comments:
Post a Comment