Manchester United imejiweka katika nafsi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya kufuatia kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Madrid mchezo ambao umepigwa usiku huu.
Danny
Welbeck ndiye alikuwa wa kwanza kuandika bao la vinara wa msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England Barclays Premier League Manchester United kwa bao la kichwa lilitokana na mpira wa kona uliopigwa na Wayne Rooney kunako dakika ya 20.
Hata hivyo Real Madrid walifanikiwa kusawazisha dakika tisa baadaye kupitia kwa Cristiano Ronaldo
kufuatia kuruka juu na kumzidi mlinzi Patrice Evra na kupiga kichwa mpira uliozama kushoto kwa mlinda mlango wa United De Gea.
Cristiano Ronaldo akifunga goli dhidi ya timu yake ya zamani kwa mpira wa kichwa uliompita mlinda mlango David De Gea.
Sir Alex Ferguson alipanga kikosi chake katika sehemu ya ushambuliaji ikiongozwa na Robin van Persie akisaidiana na Rooney na Welbeck.
Lakini baada ya kipindi cha kwanza kikosi cha United kilichokuwa ugenini kilijikuta kikirudi kuzuia zaidi kiasi mlinda mlango wao David de Gea akilazimika kufanya kazi ya ziada ya kuzuia mipira mingi ya hatari iliyo elekezwa langoni mwake.
Shujaa wa Manchester United mlinda mlango David de Gea alingara leo kwa kuonyesha uhodari wa kuzuia mipira ya hatari na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare.
Danny Welbeck akifunga bao la uongozi kufuatia kupokea mpira wa kona uliopigwa na Wayne Rooney.
.
Sir Alex Ferguson leo aliweka safu ya ushambuliaji ya mauaji kukabiliana na kigogo cha Hispania.
Robin van Persie akikabiliana na Alvaro Arbeloa.
Fabio Coentrao akipambana na Wayne Rooney katika harakati za kuwania mpira, nyuma yao ni Cristiano Ronaldo akiunyemelea mpira huo . |
Ronaldo akiungana na wachezaji wenzake wa Real Madrid baada ya kufunga goli la kusawazisha.
Danny Welbeck ndiye mchezaji wa kwanza wa kingereza kufunga goli kwa timu inayotoka katika ligi ya England katika dimba la Bernabeu tangu mara ya mwisho kufanywa hivyo na Alan Smith wa Leeds United mwaka 2001.
Smith alifunga goli katika mchezo uliopigwa March 6 2001.
Picha ya chini inamuonyesha Smith akiichezea Leeds United wakati huo akifunga goli la kwanza la Leeds lakini mwisho wa siku mchezo huo ulimalizika kwa timu hiyo ya kingereza kupoteza mchezo wakifungwa mabao 3-2.
Picha ya chini inamuonyesha Smith akiichezea Leeds United wakati huo akifunga goli la kwanza la Leeds lakini mwisho wa siku mchezo huo ulimalizika kwa timu hiyo ya kingereza kupoteza mchezo wakifungwa mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment