Stephen
Keshi amebadili mawzo yake ya kujiuzulu kutoka katika nafasi ya ukocha timu ya
taifa ya Nigeria ambapo sasa amesema kuwa ataendelea kuifundisha timu hiyo
ambayo ni mabingwa wapya wa Afrika kufuatia mazungumzo yake na waziri wa michezo
wan chi hiyo. Keshi ameiongoza Super
Eagles mpaka kutwa taji la Afrika jumapili kwa mara ya kwanza tangu katika
kipindi cha miaka 19.
Hapo kabla Keshi
kupitia redio Metro FM alisema kuwa atajiuzulu kazi yake baada ya kuipa
mafanikio Nigeria.
Hata hivyo
katika kipindi kisicho zidi masaa 24 Keshi amebadilisha mawazo yake kufuatia
mazungumzo yake na waziri wa michezo wa Nigeria Boloaji Abdullah.
Inter Milan yapigwa faini kwa kumbagua Balotelli.
Inter Milan imepigwa
faini ya euro €15,000 kufuatia baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kushangilia kwa kuimba nyimbo zenye maneno ya kadhia ya kibaguzi
wa rangi kwa mshambuliaji Mario Balotelli mwishoni mwa wiki iliyopita.
Balotelli
mwenye umri wa miaka 22, aliondoka Nerazzurri na kujiunga na Manchester City miaka
mitatu iliyopita na kujiunga tena na AC Milan mwezi uliopita uhamisho ambao
umewaacha mashabiki wake wakikosa raha.
Mashabiki wa Inter walionyesha hisia
zao za mapenzi kwa Balotelli katika mchezo wa jumapili ambao Inter iliibuka na ushindi dhidi ya Chievo mchezo uliopigwa uwanja wa San Siro lakini wengine wakionekana kushangilia kwa
maneno ya kibaguzi kiasi kupelekea klabu hiyo kuadhibiwa kutokana na tabia
iliyoonyeshwa na mashabiki wake.
Taarifa ya
mtandao wa Lega Calcio ( Chombo kinachosimamia ligi ya Italia) imesomeka kuwa
"Faini
ya EURO €15,000 imetolewa kwa Inter Milan kwa kuwa na mashabiki ambao katika
muda wa dakika 41 za kipindi cha kwanza na dakika 42 za kipindi cha pili yalisikika
maneno yakielekezwa kwa mchezaji huyo ambayo yalikuwa na lugha ya kibaguzi.
Rais wa Inter
Massimo Moratti baadaye aliibuka na kukemea aina hiyo ya ushangiliaji na
kuelezea matumaini yake kuwa Balotelli hatalengwa tena na aina hiyo ya kibaguzi
katika mchezo wa Milan derby mwishoni mwaa mwezi February.
"Nimeambiwa
juu ya hilo kwakuwa sikuweza kuelewa vizuri walikuwa wanasema nini, samahani
kwa hilo"
No comments:
Post a Comment