KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, February 12, 2013

CHAMA CHA WAAMUZI WA SOKA FRAT KUPATA VIONGOZI WAO KESHO MOROGORO. KAZI IPO KATI YA ARMY SENTIMEA NA SAIDI NASORO KITI CHA MWENYEKITI.

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) unafanyika Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FRAT walitakiwa kufika Morogoro hii leo(Februari 12) . Pia wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa mwaka 2013 kabla ya uchaguzi.

Wagombea ni Army Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.

Abdallah Mitole, Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya Mhazini inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi wanawake yupo Isabela Kapera.

Wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.

No comments:

Post a Comment