KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, March 8, 2013

JOSEPH ITANGALE MAARUFU KAMA MZEE KINESI KUKAIMU NAFASI YA KABURU NA RAHMA AL HAROUZ MALKIA WA NYUKI KUONGOZA KAMATI YA HANS POPPE USAJILI NA KAMATI YA USHINDI YA SIMBA.

Mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi akitangaza mabadiliko ya uongozi wa juu wa klabu ya Simba ikiwa ni siku moja tu baada ya Zakharia Hans Poppe na Geofrey Nyange Kaburu kubwaba Manyanga.
Kaimu mwenyekiti mpya wa kamati ya usajili na ushindi ya Simba.
 Baada ya siku moja kupita kufuatia viongozi wawili wa kamati ya utendaji ya Simba kutangaza kujiuzulu, mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi hii leo ametangaza mabadiliko ya dharura ya  uongozi wa klabu ya klabu hiyo.

Katika mabadiliko hayo mzee Kinesi amesema kuanzia hii leo nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hans Poppe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo sasa itakuwa ikishikiliwa na Bi Rahma Al Harouz( malkia wa nyuki) huku nafasi ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Geoffrey Nyange Kaburu sasa itakuwa ikikaimiwa na yeye mwenyewe.

Mabadiko hayo yamefuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba kilicho fanyika jana usiku bila ya kuwepo mwenyekiti Alhaji Ismail Aden Rage ambaye yuko nchini India akifanyiwa matibabu ambaye hata hivyo baada ya mawasiliano kufanyika alikubali na kubariki mabadiliko hayo.

Mzee Kinesi amesema kwamba kwasasa klabu ya Simba bado ina umoja na katika kipindi hiki wameunda kamati ya ushindi ambayo itakuwa chini ya Malkia wa nyuki na kwamba ni wakati wa kuondoa mipasuko ndani ya klabu hiyo.

Jioni hii uongozi wa klabu ya Simba umetembelea tawi la mpira pesa kwa lengo la kuvunja mpasuko ndani ya klabu hiyo na kujenga umoja.
BOFYA CHINI KUMSIKILIZA

No comments:

Post a Comment