KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, March 11, 2013

KUDRA OMARY NA HAMISI YUSUFU WAZIRI WA ULINZI WASHINDWA KUZIPANDISHA JKT MLALE NA POLISI IRINGA.

Mlinzi wa kati wa Zamani wa Yanga aliyepachikwa jina la 'waziri wa Ulinzi' wakati wake Hamisi Yusufu wa kwanza kulia aliyeshika chupa ya maji alikuwa ni mlinzi wa kati wa Polisi Iringa ambayo imeshindwa kupanda kucheza ligi kuu msimu ujao baada ya kushiriki ligi daraja la kwanza kutoka kundi A, Hamisi Yusufu amesema ligi daraja la kwanza ilikuwa na changamoto kubwa kwake na wachezaji wenzake kwa kuwa mkoa wa Iringa ulishindwa na wadau wa soka wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi kutokuiunga mkono timu yao katika kampeni yao ya kuipandisha timu hiyo.
Nahodha wa timu ya JKT Mlale ambaye ni mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka Afrika Mashariki na kati Yanga Kudra Omari aliyevaa kitambaa cha unahodha wa timu yake . Kudra amesema licha ya kujitolea kwa nguvu zake zote kuhakikisha anafanikiwa kuipandisha ligi kuu JKT Mlale bado dhamira yake imesindikana kutoka na kukosa sapoti ya mkoa wa Ruvuma. Mlale ilishiriki ligi daraja la kwanza kundi A ambalo lilikuwa na timu za Mbeya City, Polisi Iringa, Kurugenzi, Majimaji, Mkamba Rangers na Bukina Faso za Morogoro. 
Nahodha wa timu ya JKT Mlale ambaye ni mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka Afrika Mashariki na kati Yanga Kudra Omari aliyevaa kitambaa cha unahodha wa timu yake . Kudra amesema licha ya kujitolea kwa nguvu zake zote kuhakikisha anafanikiwa kuipandisha ligi kuu JKT Mlale bado dhamira yake imesindikana kutoka na kukosa sapoti ya mkoa wa Ruvuma. Mlale ilishiriki ligi daraja la kwanza kundi A, ambalo lilikuwa na timu za Mbeya City, Polisi Iringa, Kurugenzi, Majimaji, Mkamba Rangers na Bukina Faso za Morogoro. 

No comments:

Post a Comment