Masoud Nassor Cholo na Salum Abubakar sureboy katika mazoezi ya timu ya timu ya taifa yaliyofanyika uwanja wa taifa jana jioni(picha kutoka lenzi ya michezo). |
Masoudi Nassoro na Mbwana Samata wakifanya mazoezini uwanja wa jana Taifa. |
Washambuliaji
wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameanza mazoezi na timu ya taifa baada ya kuwasili nchini tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kundi C dhidi ya Morroco utakao fanyika jumamosi uwanja wa taifa.
Ujio
wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini
kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha
aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti
kambini leo asubuhi.
Wachezaji
John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao
walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri.
Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na
ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia
nayo wenzao kuwa imejaa.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
Kim Poulsen jana imeendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment