Timu tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kurudi Ligi ya Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika
nafasi za mwisho katika ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi
iliyopita.
Small Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada
ya kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye
moja ya mechi zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza
yalifutwa.
Moro United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka
kundi B baada ya kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi
C timu iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na
moja.
Timu zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi
31, vinara wa kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye pointi 29
wakati Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa na pointi 32.
No comments:
Post a Comment