Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere
atakuwa nje ya uwanja wa kipindi cha wiki tatu kuanzia sasa, kufuatia kupata maumivu ya
kifundo cha mguu na hivyo kupelekea kukosekana katika michezo mingine ya England kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino na Montenegro mwezi
huu.
Majeraha hayo pia yatamuweka nje
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa
Ulaya baina ya timu yake ya Arsenal dhidi ya Bayern Munich mchezo ambao
umepangwa kufanyika Jumatano.
Arsenal kwasasa iko nyuma ya Munich
kimatokeo kwa mabao mabao 3-1 yaliyopatika katika mchezo wa kwanza.
Wilshere alikumbwa na maumivu hayo ya
kifundo cha mguu wake wa kushoto katika mchezo ambao washika bunduki hao
walifungwa kwa mabao 2-1 na Tottenham Machi 3.
Itakumbukwa katika msimu uliopita
Wilshere alikosekana katika msimu mzima kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu wa
kulia.
Licha ya kucheza michezo saba tu
katika msimu huu, Wilshere anatazamwa kuwa ni kiungo muhimu katika kikosi cha
kocha wa Roy Hodgson wakati huu ambapo England ikiwa katika kampeni ya kufuzu
fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Franz Beckenbauer anamtaka Rooney.
Kigogo kutoka pande za Bavaria,
Bayen Munich kinatarajia kukaribisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United ambaye
amekuwa akizungumzwa kama mmoja wa wachezaji bora duniani.
Franz Beckenbauer anasema
angependelea Bayern Munich kumsajili Wayne Rooney.
Tetezi nyingi zimezagaa zikihusisha
hatma ya baadaye ya mshambuliaji huyo wa Manchester United baada ya kuondolewa
katika kikosi cha kwanza cha meneja Alex Ferguson katika mchezo wa pili wa vilabu
bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Franz Beckenbauer mwenye historia ya kuwa
nahodha wa Ujerumani mwenye mafanikio makubwa kwa muda mrefu amekuwa aakivutiwa
na Rooney, akimuelezea kuwa ni
"mmoja kati ya wachezaji wakubwa
sana duniani ".
"Ningefurahi Wayne Rooney ajiunge
na Bayern,".
Pep Guardiola ambaye anajipanga
kuelekea Allianz Arena kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa msimu, angependelea kupewa bajeti ya uhamisho wa wachezaji ili kujenga kikosi imara.
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amewataka
wachezaji wenzake kukaza buti na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili
kumaliza katika moja ya nafasi nne za juu na kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya.
Wekundu hao wamefanikiwa kushinda
michezo mitatu ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya Tottenham Jumapili katika dimba
la Anfield.
Gerrard anaamini ushindi utaipatia
klabu hiyo imani na kuongeza kasi ya kusonga mbele kwenye changamoto ya ligi ya
hiyo kusaka nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya.
Kwasasa Liverpool iko katika nafasi
ya sita katika msimamo wa ligi, ikiwa ni alama saba nyuma ya Chelsea wanaoshika
nafasi ya nne na ambao wanamichezo zaidi ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment