KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, April 17, 2013

FIFA KUTANGAZA HATMA YA UCHAGUZI WA TFF NDANI YA KIPINDI CHA WIKI MOJA.


Shirikisho la soka duniani fifa wiki ijayo linatarajiwa kutoa majibu ya mgogoro wa uchaguzi wa chama cha soka nchini Tanzania TFF ambapo pia litaweka wazi majibu ya nani atasimama katika uchaguzi huo.

Ujumbe maalumu wa  fifa umekamilisha kazi yake ya uchunguzi juu ya sakata hilo hilo hii leo.

Ujumbe huo ulikuwa nchini chini kwa siku mbili chini ya Primo Covarro, ambapo walikuwa wakichunguza hali ya mambo juu ya sakaa hilo ambapo liipitia mchakato mzima wa uchaguzi na kukamilisha kazi hiyo hii leo.

Akiongea na waandishi wa habari Covarro amesema "Nimekutana na kusikiliza wagombea wote walioenguliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF, maafisa wa serikali na wengine wote walihusika katika mchakato huo wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa shirikisho la soka nchini TFF".

"Sisi sio watoaji wa maamuzi, kazi yetu ni kuwasilisha ripoti Fifa na Caf, na maamuzi yatatolewa na ndani ya kipindi cha wiki moja"

Mgogoro wa uchaguzi uliibuka wakati kamati ya uchaguzi ilipowaengua wagombea kadhaa akiwemo aliyekuwa katibu wa zamani wa Yanga Jamal Malinzi.

Malinzi alikosa sifa kutokana na kukosa sifa ya kuongoza shughuli za soka ndani ya kipindi cha miaka mitano mufululizo hali iliyo sababisha nafasi ya mgombea wa nafasi ya Rais kusaliwa mgombea mmoja Athuman Nyamlani ambaye amekosa mpinzani.

Naye katibu wa zamani wa TFF Michael Wambura, ambaye alikuwa akiwania nafasi ya makamu wa Rais pia aliondolewa na kamati ya rufaa ya uchaguzi kutoka na kukosa uadilifu jambo ambalo alilipinga vikali.

Uchaguzi huo ulisimamishwa FIFA mwishoni mwa mwaka jana ambapo Rais wa sasa wa TFF President Leodegar Tenga anaendelea kuongoza mpaka hapo uchaguzi huo utakapo kamilika.

No comments:

Post a Comment