Saint George
iko katika nafasi nzuri ya kuwa timu ya kwanza kutoka Ethiopia kutinga hatua ya
makundi ya michuano ya soka ya vilabu barani.
Timu hiyo
kutoka katika jiji la Addis Ababa imefanikiwa kuichapa ENPPI ya Misri bao 2-0 katika
mchezo wa kwanza uliofanyika hii leo on Sunday ukiwa ni mchezo wa play-off ya
michuano ya kombe la shirikisho.
Shimeles
Bekele aliandika bao la kwanza la Saint George baada ya dakika nne ya mchezo
huo kuanza na Abebaw Butako kuongeza la pili dakika 22 baadaye.
Pia mabingwa
wa zamani wa vilabu Afrika TP Mazembe imepata ushindi maridhawa wa mabao 4-0 dhidi
ya Liga Muculmana ya msumbiji mchezo uliofanyika Lubumbashi.
Bao la
kwanza la Mazembe liliwekwa kimiani na raia wa Ghana Richard Kissi Boateng kunako
dakika ya 16 baada ya mpira wa kona wa Tresor Mputu Mabi.
Na baadaye
dakiki kumi kabla ya mapumziko alikuwa mzambia Given Singuluma aliyeandika bao
la pili kwa njia ya kichwa baada ya mpira wa kona wa Mputu Mabi.
Dakika nane
baada ya mapumziko mtanzania Mbwana Samatta akaandika bao la tatu baada ya
shuti la mshambuliaji Solomon Asante .
Mshambuliaji
mwingine raia wa Zambia Nathan Sinkala akaandika bao lingine la nne kufuatia Eric
Bokanga kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Hapo jana Stade
Malien ya Mali iliichapa bila huruma Lydia LB Academic ya Burundi kwa mabao 5-0
katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kusaka nafasi yakutinga hatua ya
makundi ya kombe la shirikisho.
Hii itakuwa
ni mara ya pili kwa Stade Malien kuingia hatua ya makundi endapo itafanikiwa
kutinga hatua hiyo baada ya kushindwa kufuzu michuano ya vilabu bingwa na
kuangukua katika hatua ya play-off ya kombe la shirikisho.
Mabingwa za
zamani wa Afrika Etoile du Sahel ya Tunisia wanafaida ya kutinga hatua hiyo kwa
goli la ugenini endapo itashinda mchezo wa marudhiano au kwenda sare ya bila
mabao baada ya kupata sare ya bao 2-2 dhidi ya JSM Bejaia ya Algeria mchezo
uliopigwa nchini Algeria.
Mohamed
Derrag aliandika bao la kwanza kwa wageni kunako dakika ya 26 lakini Aymen
Belaid akawasawazishia Etoile dakika 10 baadaye.
Etoile walikuwa
wakijilinda zaidi kunako kipindi cha pili lakini iliwaghararimu kunako dakika
ya 59 minutes when baada ya krosi ya Boukemacha Nassim kutengenezwa uzuri na Nabil
Ait Fergane kifuani na kuandika bao kwa wenyeji.
Mlinda mlango
wa Bejaia Djebarat Mohamed aliokoa michomo mingi ya mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Hata hivyo Etoile
wakafanikiwa kundika bao kupitia kwa Drame Michailou kunako dakika ya 86.
Ijumaa FUS
Rabat walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa jiji la
Rabat FAR Rabat huku bao pekee la washindi likifungwa na mlinzi Yassine El
Kourdi.
Mabingwa wapywa
wa Algerian Entente Setif wameichapa US Bitam kwa mabao 2-0 katika mchezo wao
wa kwanza .
Ogbi
Benhadouche aliandika bao la uongozi dakika nne kabla ya mapumziko kabla ya
mchezaji aliyeingia baaye Mohamed Amine Aoudia kuandika bao la pili kunako
dakika ya 60.
Hata hivyo Entente
Setif, inayofundishwa na bosi raia wa Togo Hubert Velud, watalazimika kumkosa Farouk
Belkaid katika mchezo mchezo wao wa pili wa marudinao mjini Bitam kufuatia
kulambwa kadi nyekundu baada ya kuzozana na mwamuzi.
Michezo ya
marudiano itachezwa kuanzia May May 31 mpaka june 2 na michezo makundi ikitarajiwa
kupigwa katikati ya mwezi Julay.
Gael Clichy aongeza mkataba Manchester City.
Mlinzi
wa pembeni wa Manchester City Gael Clichy ameanguka kwa mara nyingine tena
saini ya kuendelea kuichezea klabu hiyo mpaka mwaka 2017.
Mlinzi huyo
wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 ameichezea klabu hiyo jumla ya
michezo 74 tangu alipohamia akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho ya pauni
milioni £7 mwaka 2011.
Amenukuliwa akisema
"mambi
hayakwenda vizuri msimu huu lakini tutakuwa thabiti msimu ujao"
Clichy amekuwa
akimuweka katika benchi Aleksandar Kolarov katika michezo ya wiki za mwisho wa
msimu.
Ingawaje City
haina meneja kwasasa kufuatia Roberto Mancini kutupiwa virago jumatatu lakini
meneja wa muda Brian Kidd anasema Clichy atakuwa hazina kwa yeyeto atakaye kuja
kuchukua timu hiyo.
No comments:
Post a Comment