Mourinho anamatumaini kumchukua Ronaldo kutoka Real Madrid majira ya kiangazi. |
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amezungumzia juu ya uwezekano na mwelekeo wa Cristiano Ronaldo hapo baadaye kufuatia Jose Mourinho kuelekea Chelsea wakati huu ambapo Manchester United ikikanusha kutaka kumsajili tena nyota huyo raia wa Ureno.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 27, yuko katikati ya vita ya kuwaniwa kwa gharama ya pauni milioni £80 baada ya taarifa kuzidi kuzagaa kuwa mreno huyo kutokuyafurahia tena maisha katika mji mkuu wa Hispania Madrid.
Alipoulizwa juu ya kama mreno huyo mwenye kiwango cha juu alikuwa na furaha ndani ya Real Madrid, Calderon amesema 'Ronaldo alisema hakuwa ni mwenye furaha tangu kuanza kwa msimu. Nadhani mahusiano Rais wa sasa si mazuri, pengine kwasababu Rais hakupenda mchezaji huyo aliyemrithi.
Ronaldo amefunga jumla ya magoli 55 msimu huu katika klabu ya Real Madrid.
Vilabu vitatu vya Manchester City, PSG na
Chelsea vinatajwa kuwa na uwezo wa kumlipa mshambuliaji huyo, ambapo Calderon anasema hadhani kama kila klabu inaweza kulipa ada hiyo ya uhamisho kwa mchezaji huyo.
'Real Madrid wanaelekea kuzungumzia juu ya mkataba wake na watatoa maamuzi. Ni jambo ambalo tutalijua ndani ya wiki chache zijazo.
United walikuwa wa kwanza kujitokeza kutaka kumsajili endapo Real itaamua kumuuza ili aweze kurejea Old Trafford.
Lakini hata hivyo Mourinho, ambaye amefanya naye kazi kwa miaka mitatu ndani ya Bernabeu amemuongeza katika orodha yake ya awali.
Wayne Rooney, ambaye alionyesha kuitaka Chelsea, pamoja na mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani pia wanatakiwa na Mourinho.
Pichani juu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney (kushoto) na Edinson Cavani wa Napoli pia wanatakiwa na Mourinho
Abramovich anajipanga kumpa Mourinho pauni milioni £100 ya matumizi ya kiangazi.
Ronaldo ameitumikia Real Madrid kwa misimu minne lakini sasa anaonekana kukerwa na anakosa raha ndani ya klabu hiyo.
Ingawaje haitakuwa na uwezo wa kuwashawishi washambuliaji wote watatu kujiunga na Chelsea, klabu hiyo imedhamiria kwenda vizuri katika usajili wa kiangazi.
Mahusino ya Mourinho na Ronaldo yalikuwa katika mashaka makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mshambuliaji huyo kuonekana akipiga kelele mbele ya Mourinho kwa maneno yanayodhaniwa kuwa yalikuwa ni matusi ya ‘****
you’ baada ya kuifungia Real goli la 200.
Ronaldo inasemekana alitumia lugha ya kireno yaliyotafririwa kama ‘I’m here, I’m here’ wakati kocha huyo akiwa katika maandalizi ya kuondoka Hispania katika klabu ya Real baada ya kuifundisha kwa kipindi cha miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment