Andre
na Jordan Ayew kwa pamoja wamekubali kurejea nyumbani baada ya kufanya
mashauriano na rais wa Ghana John Mahama mjini Accra.
Ndugu hao wawili walitangaza kuwa hawataichezea
tena timu ya taifa ya Ghana mwezi Februari, baada ya kutofautiana na
wasimamizi wa timu hiyo ya taifa ya Black Stars.
Ripoti
zinasema wachezaji hao wawili wa klabu ya Marseille ya Ufaransa
walifanya mazungumzo na rais Mahama wakati alipokuwa ziarani nchini
Ufaransa.
Na katika mkutano wao wa pili, hii leo wachezaji hao waliafikiana kurejea tena nyumbani ili kuichezea Black Stars.
''Sasa tumerejea tena na tutafanya kila juhudi
ili kuhakikisha kuwa Ghana imefuzu kwa kombe la dunia'' walisema mandugu
hao wawili.
Andre Ayew, aliacha kuichezea Black Stars,
akidai kuwa hana uhusiano mzuri na viongozi wa shirikisho la mchezo wa
soka nchini humo naye Jordan hakufurahishwa na auamuzi wa viongozi hao
wa kumuacha nje ya kikosi kilichocheza nchini Afrika Kusini.
Ayew amesema wameamua kurejea tena katika timu hiyo ya taifa bila masharti yoyote.
Waziri wa michezo Elvis Afriyie Ankrah amesema
rais wa nchi hiyo aliingilia kati mzozo huo kwa sababu anaamini kuwa
timui ya taifa ya Ghana ni sharti iwe na wachezaji wake wote wenye
vipaji na walio katika hali nzuri ili kuandikisha matokeo mema.
Wachezaji hao wawili sasa watajumuishwa kwenye
kikosi cha Ghana kitakachocheza mechi za kufuzu kwa kombe la dunia dhidi
ya Zambia Septemba mwaka huu.
Hata hivyo wengi wanasubiri kuona ikiwa kocha wa Ghana Kwesi Appiah atawashirikisha wachezaji hao wawili katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment