Kocha Claude LeRoy wa DRCongo |
Claude LeRoy ameachia ngazi kama mkufunzi wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kocha huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka
65 alichukua wadhifa huo wa kuifundisha timu ya Leoards kwa mara ya pili
mwezi Septemba mwaka 2011.
"niliwambia
wachezaji wangu kwamba nitaachia ngazi baada ya miaka miwili,"alisema
Le Roy,ambaye mechi yake ya mwisho ilichezwa jumapili iliyopita dhidi ya
Cameroon.Timu mbili zilitoka sare ya bila kufungana,katika mechi za
mchujo wa kutafuta tiketi ya fainali za kombe la dunia.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR Congo
haitafuzu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 na
kama ilivyotarajiwa Timu ya taifa ya Cameroon ilipewa alama tatu baada
ya Togo kukiri kwamba mapema mwezi huu ilimtumia mchezaji ambaye
hakuruhusiwa kucheza.
LeRoy alisaidia Jamuhuri ya kidemokrasia ya
Congo kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa ya bara la Afrika mwaka
2013 nchini Afrika kusini,lakini ikashindwa kuvuka hatua ya makundi
licha ya kutopoteza mechi hata moja.
Ni kwa mara ya saba LeRoy akisaidia timu kufuzu
kwenye fainali za kombe la Afrika baada mafanikio yake akiifundisha
Cameroon na kunyakua kombe hilo mwaka 1988.Pia alizifundisha Senegal na
Ghana.
No comments:
Post a Comment