Liverpool inaendelea
na jitihada zake za mpango wa kumsajili kiungo wa Armenian Henrikh Mkhitaryan katika
moja ya usajili wao mkubwa kipindi hiki cha uhamisho wa kiangazi.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 24 huenda akaihama klabu hiyo kwa pauni milioni £20 kutoka
kwenye mkataba wake wa sasa na Shakhtar Donetsk ya Urusi.
Imeelezwa kuwa
Liverpool imeonyesha nia ya kufikia kiwango hicho.
Kiungo huyo
amekuwa mchezaji bora wa Armenia katika miaka ya 2009, 2011 na 2012 mfululizo.
Maafisa wa Anfield
wako katika hadhari ya kukumbana na upinzani wa kumpata Mkhitaryan, ambaye ameifungia
Shakhtar jumla ya mabao 25 msimu uliopita lakini pia Liverpool wanaaamini
kushinda upinzani wowote na kumshawishi kiungo huyo kujiunga nao.
Meneja Brendan
Rodgers anaona kuwa Mkhitaryan, ambaye pia amekuwa akiuhusishwa na kujiunga na Juventus
pamoja na Borussia Dortmund, kuwa usajili muhimu katika mipango yao ya kuongeza
makali ya kikosi msimu ujao.
Mkhitaryan aliaanza
kucheza soka katika klabu ya Pyunik nchini kwao Armenia ambayo aliifungia jumla
ya magoli 30 katika jumla ya michezo 70 aliyoichezea klabu hiyo.
Alielekea Ukraine
na kujiunga na Metalurh Donetsk kiangazi 2009 na baada ya kuifungia jumla ya
magoli 12 katika jumla ya michezo 37 aliyoicheza akajiunga na Shakhtar August
2010.
Mkhitaryan aliinza
kuichezea timu yake ya taifa January 2007 katika mchezo wa kimataifa wa
kirafiki dhidi ya Panama ambapo aliifungia jumla ya magoli 11 katika jumla ya
michezo 38.
Wakati huo
huo Liverpool imesalia katika mazungumzo na Sunderland kwa lengo la kumsajili
mlinda mlango Simon Mignolet.
Liverpool wameweka
mezani pauni milioni £8 ilhali Sunderland ikisalia na masimamo wa kutaka pauni
milioni £10 ambayo itamaliza zoezi hilo.
Rodgers tayari
ameshamsajili mlinzi wa Manchester City Kolo Toure na wanaendelea na mpango wa
kumsaliji mshambuliaji wa Celta Vigo Iago Aspas.
No comments:
Post a Comment