KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, June 22, 2013

Liverpool yakamilisha kumsajili mshambuliaji wa Sevilla Alberto kwa ada ya pauni milioni £6.8.



Luis Alberto and Ian Ayre
Luis Alberto akianguka saini mbele ya mkurugnezi wa Liverpool Ian Ayre.

Liverpool imekamilisha kumsajili mshambuliaji wa Sevilla Luis Alberto kwa ada ya uhamisho iliyowekwa wazi ya pauni milioni £6.8.

Mshambuliaji huyo Mhispania  mwenye umri wa miaka 20 ameingia kandarasi ya miaka minne na wekundu hao wa England.

Akikitumikia kwa mkopo kikosi cha Barcelona B, Alberto aliifungia jumla ya magoli 11 huku akitoa pasi za mwisho zilizo zaa magoli katika jumla ya michezo 38 aliyoitumikia kikosi hicho cha pili cha Catalunya.
Luis Alberto
Mshambuliaji mpya Liverpool Luis Alberto

Luis Alberto
Luis Alberto akipiga picha ya ukumbusho katika uwanja wa mazoezi wa Melwood.

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers ameumbia mtandao rasmi wa klabu ya Liverpool :
 'Wote tunafurahia kuwa Luis ameamua kujiunga na Liverpool.

'Amekuwa na rikodi nzuri ya soka na anastahili kuwa mchezaji wa Liverpool.

Hebu Tunaangalia mbele tutakakavyo fanya naye kazi na kuendeleza kipaji chake kwani amejiunga na kikosi chenye wachezaji wazuri chipukizi ndani ya klabu yetu.'
Luis Alberto
Alberto amesaini mkataba wa miaka minne na Liverpool baada ya klabu yake ya Sevilla kukubali kitita cha pauni milioni  £6.8.

Liverpool pia imekubali mshambuliaji wa Celta Vigo Iago Aspas ikiwa ni pamoja na mpango wa kumchukua mlinda mlango wa Simon Mignolet.
Simon Mignolet
 Iago Aspas
Mlinda mlango wa Sunderland Mignolet (pichani juukabisa) na mshambuliaji wa Celta Vigo Iago Aspas (picha ya chini) wote wanatazamiwa kujiunga na Liverpoo.

No comments:

Post a Comment