KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 10, 2013

Luis Suarez anasema kuna vilabu viwili au vitatu vinataka kumnunua.Christian Benteke awasilisha ombi la kuondoka Aston Villa. Sunderland imemsajili kinda wa ufaransa.Leonardo ajiuzulu kazi ya ukurugenzi wa soka PSG baada ya kifungom cha msimu.


Luis Suarez anasema kuna vilabu viwili au vitatu vinataka kumnunua.
 Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amesema kuwa ana chaguo mbili au tatu juu ya hatma yake ya kisoka
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anataka kuondoka katika klabu yake hiyo na amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal, ambayo tayari imeweka mezani pauni milioni £30.
Suarez anatarajiwa kurejea Anfield tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya July 21 na kwamba mamabo yanaweza kubalika wakati wowote

Christian Benteke awasilisha ombi la kuondoka Aston Villa.
 Nyota wa Aston Villa Christian Benteke amepeleka rasmi ombi lake la kutaka kuihama klabu yake lakini klabu yake hiyo bado inaonyesha kuendelea kusalia naye.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 alisani na klabu yake akitokea Genk kwa ada ya uhamosho ya pauni milioni £7 msimu uliopita na kuifungia jumla ta mabao 23 katika michuano mbalimbali.

Villa imemuambua Benteke, ambaye amekuwa akihusishwa na kuelekea  Arsenal, Chelsea na Tottenham, watashughulisha na ofa ambayo itawapendeza .
Benteke raia wa Congo hajasafiri na klabu yake katika ziara ya pre-season kule ujerumani lakini Villa imesema kuwa imempa mpaka muda mpaka July 18 kabla ya ombi lake kufanyiwa kazi.

Sunderland imemsajili kinda wa ufaransa.
 Sunderland imemsajili kiungo El Hadji Ba baada ya kuondoka Le Havre.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa huru baada ya kuondoka Le Havre msimu uliopita ambako alifunga goli moja katika jumla ya michezo 13.
Ba anajiunga na Jozy Altidore, David Moberg Karlsson, Cabral, Modibo Diakite, Valentin Roberge na Duncan Watmore katika viunga vya Stadium of Light.

Leonardo ajiuzulu kazi ya ukurugenzi wa soka PSG baada ya kifungom cha msimu.
 Leonardo amejiuzulu katika nafasi yake kama mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris St-Germain na anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa mwezi ujao wa August.
Kiungo huyo wa zamani wa Brazil mwenye umri wa miaka 43, alisimamishwa kwa miezi tisa kwa kitendo cha kumsukuma mwamuzi mwezi May.
Baadaye akaongezewa adhabu nyingine ya kusimama katika shughuli za soka kipindi cha miezi 13 adhabu ambazo zitamuweka nje ya soka mpaka msimu ujao lakini sasa akiamau kuondoka.

No comments:

Post a Comment