Madrid yaahirisha mpango wa uhamisho wa Higuain sasa kutokwenda tena Arsenal |
Arsenal inakabiliwa na vita kubwa ya kumnasa Gonzalo Higuain kutoka katikam klabu ya Real Madrid baada ya taarifa kusema kuwa kigogo cha Hispania, Madrid kitaondoa wazo la ada kuwa ilikuwa inahitajika kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Argentina.
Licha ya kuwepo na tetesi kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huenda kaelekea London ya Kaskazini taarifa zaidi zinasema hakuna makubaliano baina ya vilabu hivyo viwili wakati huu wa kipindi kirefu cha uhamisho wa wachezaji cha Kiangazi.
Kuwasili kwa Carlo Ancelotti kama bosi mpya wa Real kulidhaniwa kuwa kungekuwa ni chachu ya uhamisho lakini magazeti ya Hispania sasa yameibuka na taarifa inayosema Higuain huenda sasa akaelekea kusalia Bernabeu.
Hapo kabla alithaminishwa kwa pauni milioni £23 mpango ambao sasa unaonekana kuyeyeka na kwamba Real bado haijaweka bayana kiwango rasmi kwa ajili ya Higuain kuhama,
jambo ambalo linaonekana kama limemzuia mzee Arsene Wenger.
Baba yake na Higuain alinukuliwa mapema wiki hii akisema uhamisho wa mwanawe huenda ukakamilika muda si mrefu lakini taarifa za nchini Hispania zinaonyesha kuwa inataka kusalia kuwa naye
Baba yake na mshambuliaji huyo Nicolas alinukuliwa akisema kupitia mtandao mmoja nchini akisema.
'Endapo anajiunga na Juve, na mpango wa Higuain kuelekea Arsenal uko karibu.
'Juventus ni klabu kubwa lakini Gonzalo ni mwenye thamani kubwa kwao.
'Napoli ni timu imara. sitakanusha kuwa Gonzalo karibu anajiunga na Arsenal.'
Arsenal pia wako vitani kunasa saini ya mchezaji wa Fiorenrtina Stevan Jovetic
No comments:
Post a Comment