Hatimaye ndoto za safari ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuelekea katika fainali za michuano ya wachezaji wa ndani barani Afrika sasa zimeyeyuka kufuatia kukubali kichapo cha pili cha mchezo wa marudiano kutoka kwa timu ya taifa ya Uganda maarufu kama Uganda Cranes.
Stars iliyochini ya kocha Kim Poulsen imeondoshwa mashindanoni baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Namboole maarufu kama Uwanja wa Mandela jijini Kampala nchini Uganda.
Hicho ni kichapo cha pili kwa Stars baada ya kukubali katika uwanja wake wa nyumbani wiki mbili zilizopita ambapo ilivyolewa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uganda Cranes sasa imefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo ambayo itapigwa nchini Afrika kusini mwkani.
Waganda itabidi waashukuru wafungaji wa mabao hayo Frank Kalanda na goli lingine kwa njia ya penati la winga wa KCC Brian Majwega na hivyo kupata ushindi wa jumla wa mabao 4-1.
Bao pekee la Stars lilifungwa na kiungo Amri Kiemba.
Katika michezo mingine Mali imesonga mbele baada ya kuichapa Guinea bao 3-1 katika uwanja wa nyumbani kama ilivyo kwa Sudan baada ya kulazimisha sare ugenini nchini Burundi sare ya bao 1-1 nayo imesonga mbele.
Burkina Faso na mabingwa wa mwaka 2009 Democratic Republic of Congo watakuwa na vibariavigumu dhidi ya Niger na Congo-Brazzaville baada ya timu zote hizo kupata ushindi kiduchu wa bao 1-0 katika viwanja vyao vya nyumbani.
Pia kutakuwa ni michezo kadhaa ambayo itakuwa ikipigwa kama michezo ya kwanza ambapo Cameroon baada ya kupona adhabu ya shirikisho la soka dunia FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kushutumiwa na FIFA kuingilia soka la nchi hiyo, sasa watakuwa wakiwakaribisha Gabon katika jiji la Younde.
Kusini mwa bara la Afrika Botswana watakuwa wenyeji wa Zambia, Mozambique dhidi ya Namibia nao Mauritius watakuwa wakikamilisha mchezo wa 11

No comments:
Post a Comment