Klabu ya soka ya Internacional ya nchini Brazil imeviambia vilabu vya Tottenham na Southampton kuwa watatakiwa angalu kulipa pauni milioni £22 ili kumsajili mshambuliaji wake Leandro Damiao.
Vilabu vyote Spurs na Southamton vimekuwa vikifuatialia saini ya Damiao kwa udi na uvumba kiangazi hii baada ya mshambuliaji huyo kutamka kuwa anapenda kucheza katika ligi kuu ya soka nchini England Premier League.
Hata hivyo mkurugenzi wa Internacional Marcelo Medeiros amevionya vilabu hivyo vinavyo muwania Damiao wasielekee kwao wakidhani kuwa mshambuliaji huyo ni wa bei rahisi.
Amenukuliwa na gazeti la Globo akisema
‘Bei ya Damiao ni pauni milioni £22million kama kuna klabu ambayo inamtaka Damiao, hiyo ndiyo bei yake.’
Tayari Dejan Lovren na Victor Wanyama wameshatua kwa hela nyingi lakini inaarifiwa kuwa Damiao huenda akawa na gharama ya juu kuliko wote.
Napoli iliweka wazi mapema mwezi huu kuwa wanamtaka mshambuliaji huyo lakini walibadilisha nia na kuelekeza nguvu kwa Gonzalo Higuain na mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez.
No comments:
Post a Comment