Jose Mourinho anasema bado hajakata tamaa
katika jitihada zake za kutaka kukamilisha usajili wa Bertrand Traore
anayejaribiwa katika ziara ya timu hiyo ambaye anasema mchezaji huyo anaweza
kuchezea kikosi cha kwanza cha timu yake.
Traore, Nyota Kijana wa Kutoka
nchini Burkina Faso kimataifa, amekuwa nyota ya ziara ya Chelsea iliyo katika
ziara ya kuanza msimu barani Asia baada ya kufunga mabao mawili katika mechi
tatu.
Traore mwenye umri wa miaka 17 amekwenda
katika ziara hiyo baada ya kutakiwa na Mourinho kwenda naye na anasema
hatachoka kufanya kazi ya kuhakikisha anakamilisha mipango ya kumsajili.
Traore ambaye amekuwepo katika
kikosi cha Chelsea cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 katika kipindi
cha miaezi 18 lakini inakuwa ngumu kuidhinishwa katika kikosi cha kwanza baada
ya kukabiliwa na kunyimwa kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza
Hata hivyo, Mourinho anasema mipango
ya kukamisha usajili wake itakamilishwa kabla ya tarehe yake ya kuzaliwa mwezi
ujao ambapo atakuwa anakamilisha umri wa miaka 18 na moja kwa moja atamuingiza
katika kikosi cha kwanza
Traore amevutia ziara ya anasema Mourinho.
No comments:
Post a Comment