Mshambuliaji Arouna Kone |
Timu ya Newcastle inatafuta kwa udi na uvumba kuapata siani ya mshambuliaji wa Wigan Arouna Kone.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29
alishinda magoli 11 katika ligi kuu ya England na kushinda kombe la FA
lakini anataka kuihama timu hiyo baada ya kushushwa daraja.
NewCastle ina upinzani wa Evarton ambayo nayo
imekuwa ikitaka kumsajiri.Lakini Meneja wa Wigan Owen Coyle amesema
mshambuliaji huyo kutoka IvoryCoast , yeye anagependelea kuhamia
Everton.
"Ninaamini kupitia mwakilishi wake kuwa Everton ndiko anakotaka kuhamia"alisema Coyle.
Arouna Kone alisaini mkataba wa miaka mitatu
alipojiunga na Wigan kutoka Levante ya Uhispania msimu uliopita na
alikuwa kwenye kikosi kilichonyakua ushindi mkubwa wa kwanza kwa timu
hiyo,waliposhinda Manchester City goli 1-0 katika fainali ya kombe la FA
mwezi Mei mwaka huu.
Ryan Giggs sasa kocha mchezaji wa United huku Phil Neville akipewa kazi ya ukocha wa kikosi cha kwanza.
Manchester
United imemtangaza Ryan Giggs kuwa kocha mchezaji huku Phil Neville akitarajiwa
kutangazwa kuwa kocha wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Giggs ambaye
anatarajiwa kufikia umri wa miaka 40 mwezi Novemba na mchezaji mwenzake wa
zamani wa klabu hiyo Neville ambaye kwasasa ana umri wa miaka 36 ndio nyongeza
mpya ya kocha mpya David Moyes katika safu ya watu wake wa pembeni katika
benchi la ufundi Old Trafford.
Amekaririwa
Moyes akisema
"Nimefurahi
kwamba Ryan amekubali nafasi hiyo ya kuwa kocha mchezaji".
Kwa upande
wake Giggs ameongeza kwa kusema
"Siyo
siri nilikuwa nikichukua ujuzi wangu. Naliona hili kama ni hatua yangu ya
mwanzo kwa hatma yangu ya baadaye katika soka"
Ilitazamiwa kuwa
klabu hiyo ingemtangaza Nevile mwenye umri wa miaka 36 kuwa kocha mpya wa
kikosi cha kwanza kufuatia kuondoka klabu hapo kwa Rene Meulensteen.
Giggs amendelea
kwa kusema
"Ni
fahari kubwa kuajiriwa kama kocha mchezaji. Nina matumaini nitaweza kuleta
ujuzi wangu karibu, nikifanya kazi kama mchezaji na sehemu ya familia ya Manchester
United kwa kipindi kirefu.
"Naangalia
mbele kufanya kazi sambamba na David na timu"
Moyes ambaye
alitajwa na mtangulizi wake Sir Alex Ferguson mwezi Mei, atafanya mkutano wake
wa kwanza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza hapo kesho Ijumaa kama
meneja.
Kiungo Giggs
alisaini mkataba mwingine wa kuongeza msimu mwingine wa mwaka mmoja kama
mchezaji ndani ya United mwezi machi, mkataba ambao utamuweka Old Trafford mpaka Juni 2014 ambapo
atakuwa akikamilisha misimu 23 ya kuitumikia klabu hiyo.
Pengo la Tevez Manchester City kuzibwa na Alvaro Negredo wa Sevilla.
Manchester
City imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania Alvaro
Negredo kuziba nafasi ya Carlos Tevez baada ya kutimkia Juventus.
Negredo
mwenye umri wa miaka 27, amekadiriwa kwa thamani ya pauni milioni 24 huku City wakiwa
na matumaini ya kumnasa kwa thamani pungufu ya hiyo.
Atletico
Madrid walikuwa na mpanago wa kumchukua Negredo, lakini meneja mpya wa City Manuel
Pellegrini ameweka wazi kuwa huyo ndiye mchezaji satahili kuziba pengo la Tevez.
Everton na West
Ham hivi karibuni nao walikuwa wameonyesha nia lakini mshambuliaji huyo
alidhihirisha kuwa ni wa thamni kubwa kwa vilabu vyote viwili.
Fernandinho na
Jesus Navas tayari wameshawasili wakitoka katika vilabu vya Shakhtar Donetsk na
Sevilla majira haya ya kingazi wakati City wakiimarisha kikosi chao kwa ajili
ya kuchukua taji la ligi kuu ya England waliloliacha kwa Manchester United
msimu uliopita.
Manchester
City pia imekuwa ikihusihswa na mshambuliaji wa Benfica Oscar Cardozo katika harakati zao za
kuimarisha kikosi chao katika sehemu ya ushambuliaji baada ya kumuuza Mario
Balotelli alielekea AC Milan ya Italia mwezi Januari.
Sergio
Aguero amekubali mpango wa muda mrefu na Etihad, wakati ambapo inaaminika kuwa Pellegrini
anataka kufanya kazi na Edin Dzeko ambaye hakuwa na wakati mzuri chini ya
meneja aliyetangulia Roberto Mancini msimu uliopita.
Mchezaji wa zamani wa Brazil ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leonardo afungiwa msimu mzima.
Mkurugenzi
wa michezo wa klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa Leonardo Nascimento de
Araújo, maarufu kama Leonardo ambaye alikuwa kikaangani kwa kosa la kinidhamu
kufuatia kumsukuma mwamuzi adhabu yake sasa imeongezeka na kufikia kusimama kwa
miezi 13 ambayo ni wazi itamuweka pembeni kujishughulisha na soka kwa kipindi
chote cha msimu ujao.
Kiungo huyo
wa zamani wa Brazil mwenye umri wa miaka 43, hapo kabla alifungiwa kwa miezi
tisa adhabu iliyotangazwa mwezi Mei.
Leonardo alionekana
katika picha akitumia bega lake kugusana kwa lengo la kumsukumiza Alexandre
Castro kufuatia kukasirishwa na kadi nyekundu aliyoonyeshwa Thiago Silva katika
mchezo baina ya PSG na Valenciennes uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Alikata
rufaa lakini kwasasa amefungiwa kujishughulisha na shughuli zote za kiofisi
mpaka juni 30 2014.
Leonardo
ambaye aliwahi kusimamishwa kwa kusimama katika mstari wa unaogawa uwanja
katika moja ya michezo ya PSG anatarajiwa sasa kurejea kazini mwezi February lakini
kwasasa ataukosa msimu mzima.
Sambamba na
adhabu hiyo, klabu hiyo ambao ni mabingwa wa Ufarasna wamekumbwa na adhabu ya
kupokwa alama tatu katika kampeni ya ligi ya msimu ujao wa 2013-14.
Leonardo
ambaye alikuwa kikosini wakati Brazil ikishinda taji la kombe la dunia mwaka 1994,
amekanusha kumsukuma mwamuzi lakini hata hivyo alionekana na hatia ya kufanya
hivyo huku ajitetea kwa kusema afisa mwingine aliyekuwa karibu yake kwa bahati
mbaya alimsukuma kuelekea kwa mwamuzi Castro.
Mabingwa hao
wa ligi ya Ufaransa PSG wamemwajiri Laurent Blanc kuwa bosi mpya mwezi uliopita
baada ya Carlo Ancelotti kuelekea Real Madrid.
TANZANIA NA ENGLAND ZASHUKA VIWANGO VYA UBORA VYA FIFA, HUKU BRAZIL IKIPANDA KWA KASI YA AJABU
England imeshuka
katika viwango vya ubora vinavyo tambuliwa na fifa mpaka nafasi ya 15 kwa
mujibu wa viwango vipya vya ubora ikiwa ni nafasi ya chini kutokea tangu
waliposhindwa kufuzu kwa michuano ya Ulaya ya mwaka 2008
Kushuka huko
kwa nafasi sita kuna maanisha kuwa kikosi cha meneja Roy Hodgson sasa kimepitwa
na Bosnia-Herzegovina, Ivory Coast na Greece katika msimamo wa ubora wa viwango
vya soka duniani.
Scotland
imepanda kwa nafasi 24 mpaka kufikia nafasi ya 50 wakati ambapo Ireland ya
Kaskazini imepanda kwa nafasi tano kutoka katika nafasi ya 111 ya mwezi Juni
Wales imeshuka
kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 46 na Jamhuri ya Ireland ikishuka kwa nafasi
tatu mpaka nafasi ya 44.
Wakati hayo yakiwa hivyo soka la tanzania limeshuka kwa nafasi tatu baada ya kupungukiwa alama 12 na sasa inashika nafasi ya 35 kwa mwezi huu wa Machi tofauti na ilivyokuwa mwezi wa juni ambapo ilikuwa imeshika nafasi ya 32.
Tanzania imepoteza alama nyingi za mwezi uliopita kufuatia kufungwa katika michezo miwili muhimu ya kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia.
Stars ilifungwa na Morocco kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika nchini Morocco kabla ya kufungwa na Ivory Coast katika mchezo mwingine uliofanyika Tanzania.
Katika hali iliyotazamiwa na wengi ni kwamba Brazil imepanda kwa kasi kubwa kutoka nafasi ya 15 iliyokuwepo mwezi uliopita mpaka kufikia nafasi ya 9 mwezi huu.
Matokeo mazuri ya kupanda kwa Brazil yametokana na mafanikio iliyo yapata katika michezo ya kuwania kombe la shirikisho pamoja na michezo yake ya hivi karibuni ya kimashindano na kirafiki.
Kwa upande
wa soka la wanawake, England imepanda kwa nafasi moja ikishika nafasi ya saba
huku Scotland wakipanda mpaka nafasi ya 21. Wales kwasasa wako katika nafasi ya
37 huku Ireland ya kaskazini ikishika nafasi 54.
Bofya msimamo kamili kulia fifa Ranking.
No comments:
Post a Comment