Mlinzi wa
kati aliyekuwa anawindwa na Barcelona Thiago Silva amesaini mkataba mwingine
wa nyongeza na klabu yake ya nchini Ufaransa ya Paris St-Germain.
Mlinzi huyo
wa kati alijiunga na mabingwa hao wa ligi ya Ufaransa mwaka 2012 kwa ada ya
uhamisho ya pauni £36m, kwa mkataba wa
miaka mitano na sasa akitarajiwa kumaliza mkataba huo mwaka 2018.
Barcelona ilikuwa
ikitarajiwa kumsajili nyota huyo wa
kimataifa mwenye umri wa miaka 28 raia wa Brazil lakini suala la maslahi
limeendelea kumbakisha ndani ya klabu yake ya PSG.
Mlinzi mkongwe
wa Barca Carles Puyol mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na matatizo
ya mguu tangu mwezi March, wakati ambapo mlinzi Gerard Pique, Adriano Correia na
Javier Mascherano wamekuwa mareruhi.
Barcelona imekuwa
ikihusishwa na mlinzi mwingine wa kimataifa wa Brazil kutoka klabu ya Chelsea David
Luiz, lakini mwezi Juni wakakanusha kuwa hawakuwa katika mawindo ya kumsajili
mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 wakati huo Tito Vilanova akiwa katika
benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment