Mshambuliaji
wa Tottenham Gareth Bale ameweka wazi kuwa anataka kyuongea na wakuu wa Real
Madrid, lakini pia mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akiendelea kuweka wazi kuwa
mshambuliaji huyo raia wa Wells hatauzwa.
Real bado
hawajaweka mezani ombi maalum la kumtaka mshambuliaji huyo yaani kuweka ofa yao
mezani ambapo Spurs wakitaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kusalia
ndani ya klabu hiyo hata kama watapokea ofa hiyo inayodhaniwa kufikiwa pauni
milioni £85.
Tottenham wana
imani kuwa watafanikiwa kumshawishi Bale kumalizia mwaka wake mmoja ulisalia
ndani ya mkataba wake wa miaka mitatu.
Bale alijiunga
na Spurs akitokea Southampton mwaka 2007 kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £10.
Tamwimu za
Bale ndani ya Spurs kila mwaka.
2012-13: Played 33, scored 21, assisted 4
2011-12: Played 36, scored 9, assisted 10
2010-11: Played 30, scored 7, assisted 1
2009-10: Played 23, scored 3, assisted 5
2008-09: Played 16, scored 0, assisted 0
2007-08: Played 8, scored 2, assisted 0
Real wanatarajia
kuweka wazi nia yao wiki ijayo na kupambana na pingamizi la Tottenham ambaye
ameifungia klabu yake magoli 26 katika michuano mbalimbali msimu uliopita.
Tottenham iliwasili
London Jumapili baada ya mchezo wao wa mwisho katika ziara ya kuanza msimu
mjini Hong Kong. Bale hakucheza mchezo hata mmoja katika michuano ya Asia
Trophy ikiarifiwa kuwa alikuwa ni mwenye maumivu ya misuli.
No comments:
Post a Comment