Luis Suarez hajawasiliana na uongozi wa Liverpool juu ya hatma yake ya baade licha ya kunukukuliwa akisema
"For now, due to all of the people's affection, I will be staying."
Soma mfululizo wa taarifa juu ya Suarez na hatma yake ndani ya Liverpool kwa ufupi.
May 29: Alidokeza kuwa anataka kuondoka katika klabu ya Liverpool baada ya kusema anaona maisha nchini England ni magumu.
June 12: Suarez akaweka wazi kuwa ana mapenzi makubwa na Liverpool, lakini akasisitiza kuwa maisha nchini England ni magumu.
July 8 : Liverpool ikatupilia mbali ombi la pauni milioni £30 kutoka katika klabu ya Arsenal la kumtaka Suarez.
July 24: Arsenal ikatangaza ofa nyingine ya pauni £40,000,001 kwa ajili ya Suarez, wakichochea kwa lengo la kuvunja kifungu kinacho mbana cha mkataba wake.
August 2: Akasema atafikiria juu ya kuwasilisha rasmi ombi lake ndani ya klabu la kutaka kuondoka na kama kuna uwezekano wa kulipeleka suala lake mahakamani endapo Liverpool haitafanya maamuzi.
August 7: Suarez akasema anataka kuondoka Liverpool na kujiunga na klabu ambayo itashiriki ligi ya mabingwa Ulaya.
August 8: Akaambiwa na meneja wake Brendan Rodgers, kuwa afanye mazoezi peke yake kwani alionyesha dharau kambini.
August 8: Mmiliki w Liverpool John W Henry akasisitiza kuwa mshambuliaji Luis Suarez hatauzwa kiangazi hii na bila kujali kwa bei gani.
Mshambuliaji huyo anatarajiwa kurejea kambini ijumaa baada ya kufunga goli katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao walishinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Japan mjini Rifu hii Jumatano.
Taarifa za hivi punde kutoka katika vyombo vya habari kutoka kwa mwandishi wa habari aliye karibu sana na mshambuliaji huyo zinasema kupitia gazeti la El Observador zimesema Suarez anaweza kusaini mkataba mwingine.
Suarez, ambaye alijunga Liverpool akitokea katika klabu ya Ajax kwa ada ya uhamishi ya pauni milioni £22.7 mwezi January 2011, aliifungia Liverpool jumla ya mabao 30 baada ya kuichezea jumla ya michezo 44 msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment