KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 1, 2013

Roberto Soldado atua Spurs kwa pauni milioni £26.2.

Tottenham imetangza kuwa imemsajili mshambuliaji wa Valencia Roberto Soldado baada ya mshambuliaji huyo kufanikiwa katika vipimo vyake vya afya.

Spurs italipa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni  milioni £26.2 kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye kimsingi wamekubalina juu ya maslahi binafsi kwa kipindi cha miaka minne.

Tottenham imeweka wazi hilo kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter.
 
‘Tunafurahishwa kuwa tumefikia makubaliano na Valencia kwa ajili ya uhamisho wa Roberto Soldado baada ya zoezi la afya kufanikiwa.’

‘Mshambuliaji huyo ameifungia timu yake ya zamani jumla ya magoli 80 katika jumla ya michezo 146 katika muda wote aliokuwepo Mestalla ambako alijiunga akitokea Getafe mwaka 2010, baadaya kuwa katika kiwango safi kwa kufunga jumla ya magoli 29 baada ya kucheza jumla ya michezo 60 ya ligi.
Spurs land Soldado in £26m record deal
Roberto Soldado (Picture: Getty Images)
‘Soldado alianza kucheza soka la kuonekana katika kikosi cha pili cha klabu ya Real Madrid ambako alifunga jumla ya magoli 63 baada ya kuichezea jumla ya michezo 120, baadaye akaelekea kwa mkopo Osasuna katika msimu wa 2006-7 ambako alifunga jumla ya 11 kufuatia kuichezea michezo 30 kabla ya kuijunga na Getafe mwaka2008.

‘Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ameitumikia Hispania katika michezo 11 na kufunga jumla ya magoli sita huku mchezo wa hivi karibuni ukiwa ni mchezo ya michuano ya Confederations ilifanyika nchini Brazil mwezi June.’

Kuwasili kwa Soldado kutapandisha tetesi za usajili kwa mshambuliaji mwenzake Emmanuel Adebayor, ambaye amekuwa akihusishwa na kuelekea nchini Uturuki katika klabu ya Besiktas, kama ilivyo kwa mshambuliaji wa kimataifa wa England Jermain Defoe.

No comments:

Post a Comment