KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 24, 2013

TANZIA KATIKA SOKA LA MALAWI WACHEZAJI 3 WA LIGI KUU WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI.

Wachezaji watatu wanaochezea ligi kuu ya nchini Malawi wamefariki dunia dunia kutokana na ajali ya gari ambayo impelekea majeruhi watatu wambao wako katika hali mbaya ambao wamelazwa katika hospitali moja nchini humo.
Wachezaji hao wa timu ya jeshi ya Malawi Defence Force (Mafco) walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kuadhibiwa kutokana na utovu wa nidhamu wakati wakiwa safarini kuelekea katika mchezo wa ligi.
Dhahma hiyo inakuja saa 24 baada ya Mafco kupoteza mchezo wao kwaq penati dhidi ya timu nyingine ya jeshi ya Moyale Barracks, katika michuano ya Carlsberg Cup.
Walinzi Chifuniro Phiri, Gift Mphonde na Sadan Mangwere wote wamekufa papo hapo huku Gift Soko, Cyrus Phiri na Jimmy Nzunga wote wakiwa katika hali mbaya hospitali.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Chitumbo Chirambo amesema jumla ya wachezaji wake sita walitakiwa kurejea nyumbani wakati wakiendelea na mazoezi wakijindaa na mchezo wa mwisho wa juma kwa kunywa pombe usiku mwingi na kujisahau kuwa walikuwa kambini.

No comments:

Post a Comment