KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 24, 2013

Tom Saintfiet kumshitaki Stephen Keshi FIFA kutokana na kubagua kwa rangi.

Kocha wa timu ya taifa ya Malawi Tom Saintfiet anataka kumshitaki kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi kw shirikisho la soka duniani kufuatia kumbagua kwa asili yake akimwita "a white dude who should go back to Belgium".
Wawili hao walikuwa wakitupiana maneno tangu Malawi ilipotaka mchezo wao wa kuwania kufuzu kombe la dunia kuhamishwa katika mji wa Calabar kutokana na matatizo ya kiusalama.

Saintfiet amesema haikubiliki hata kidogo kuambiwa maneno ambayo ni wazi yana ubaguzi.

"Ni hakika kabisa kwa asilimia 100% kuwa mwanasheria wangu atalipeleka hili Fifa." 

Rapsha hiyo ilianza pale chama cha soka nchini Malawi kilipoandikia barua kwa fifa kikitaka mchezo baina yao wa kundi F uliopangwa kufanyika septemba 7 ungechezwa nje ya uwanja wa nyumbani wa Super Eagles hatua ambayo imetafririwa kwamba Malawi ambao wako nyuma ya Nigeria kwa alama mbili wana hangaika kupata matokeo mazuri ya kuweza kusonga mbele na kutinga fainali ya kombe la dunia katika mchezo huo wa play-offs.
 

No comments:

Post a Comment