Angel Di Maria ametanabaisha kuwa aliaamua kusalia katika klabu yake ya Real Madrid baada ya kufanya mazungumzo ya kina na mshambuliaji mwenzake raia wa Argentina ambaye pia ni mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Ezequiel Lavezzi pamoja na kocha wake Carlo Ancelotti.
Winga huyo mjanja alikuwa akihusishwa na kutaka kuihama Santiago Bernabeu mapema kiangazi iliyopita lakini hatimaye akaamua kusalia na kuendeleza upinzani mkali wa nafasi ya kucheza ambao haukumuogopesha.
Akiongea na Rock and Pop radio Di Maria amenukuliwa akisema
"Niliamua kusalia, licha ya ujio wa wachezaji ndani ya klabu"
"Niliamua kusalia, licha ya ujio wa wachezaji ndani ya klabu"
"Nilijua kuwa nilikuwa nikielekea katika kipindi kizuri na ambacho nilikuwa na uwezo wa kucheza hapa. Niliongea na Pocho [Ezequiel Lavezzi] na kuniuuliza 'Hivi kweli unataka kuondoka hapa?'
"Kocha Carlo Ancelotti aliniambia kuwa yoyote aliye bora atacheza. Nadhani Bale hajafanya mazoezi Tottenham hivyo nadhani nitaanza naye."
Nyota huyo wa zamani wa Benfica pia alifanya mazungumzo na Gonzalo Higuain juu ya kutaka kuondoka Madrid na kuelekea Napoli na kusema kuwa vyombo vya habari nilichangia sana juu ya tetesi za kutaka kuondoka kwake majira ya kiangazi.

No comments:
Post a Comment