Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alichukua nafasi kutoka kwa mtangulizi wake Jurgen Klinsmann mwaka 2006,
na alikuwa na mkataba mpaka kufikia fainali ya kombe la dunia 2014 lakini ameiongoza Ujerumani salama mpaka kupata nafasi nchini Brazil lakini sasa atasalia katika kibarua mpaka kiangazi 2016.
Rekodi yake Joachim Low
- P: 99
- W: 68
- D: 16
- L: 15
- Tournament record: Euro 2008 final, World Cup 2010 and Euro 2012 semi-finals
Meneja wa kikosi Oliver Bierhoff na kocha wa magolikipa Andreas Kopke pia wamesaini mkataba wa miaka miwili.
No comments:
Post a Comment