Bondia selemani Kidunda kulia naye anashiriki |
Mashindano ya ndondi ya ubingwa wa dunia yanazidi kupamba moto mjini Almaty, Kazakhstan.
Kufikia sasa ni mabondia wawili tu wa Afrika,
Efetobor Apochi wa Nigeria uzani wa heavy na Colin Louis wa Mauritius
ambao wameshinda mapigano yao na wengine sita kutoka Kenya, Misri,
Angola na Nigeria wakashindwa.
Efetobor alimshinda kwa pointi Seyda Keser wa Uturuki naye Louis akamchapa kwa pointi pia Khatuev Salavat wa Norway.
Mabondia sita walioshindwa ni Dan Shisia uzani
wa heavy, John Kariuki uzani wa light na Dennis Okoth uzani wa
light-welter wote wa Kenya, Vivaldo Rodrigues wa Angola uzani wa fly,
Olayinka Yusuff wa Nigeria uzani wa fly na Mohammed Eslam wa Misri uzani
wa light-welter aliyeshindwa na Yves Ulysse wa Canada.
Shisia alichapwa na Jim Andreasen wa Denmark kwa pointi, Kariuki akashindwa na Dorjnyambuu Otgondalai wa Mongolia.
Bondia huyo wa Kenya alipata jeraha juu ya jicho lake la kulia hivyo basi refarii akaamua hawezi kuendelea.
Mashabiki wa ndondi mjini Almaty waliachwa
vinywa wazi wakishangaa vile bondia wa Uturuki Fatih Keles alivyomshinda
Okoth kwa pointi 2-1.
Makocha wa Kenya Albert Matito na George
''Foreman’’ Onyango wanasema mashabiki waliwazomea majaji kwa uamuzi huo
wakisema bondia wa Kenya alistahili kushinda kwa sababu alimlemea
mwenzake raundi zote.
Vivaldo Rodrigues wa Angola alishindwa kwa
pointi na Malik Jackson wa Marekani uzani wa fly, na bondia mwingine wa
Nigeria Olayinka Yusuf akashindwa na Charlie Edwards wa England uzani wa
fly.
Jumatano wiki hii Raytoin Okwiri wa Kenya na
Selemani Kidunda wa Tanzania, wote uzani wa welter, wataingia ulingoni
kwa mapigano yao ya kwanza. Okwiri anazipiga na Daniel Lewis wa
Australia huku Kidunda akipambana na Mandeep Jangra wa India…
No comments:
Post a Comment