KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 11, 2013

Al Ahly klabu bingwa Afrika na vurugu kawaida yao.

Klabu ya Al Ahly ya Misri imeshinda taji la klabu bingwa Afrika ilipoicharaza Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mabao 2-0 katika mkondo wa pili na wa mechi ya mwisho mjini Cairo Jumapili.
Ahly, waliojinyakulia kombe hilo kwa mara ya saba walipata alama 3-1 kwa ujumla.
Kulikuwa na ripoti za vurugu kuzuka kati ya mamia ya wafuasi wa Ahly na polisi nchini Misri, kabla ya mchezo kuanza kuanza.
Pindi vurugu zilipositishwa, mchezaji gwiji, Mohamed Aboutrika ndiye aliyeingiza bao la kwanza katika dakika ya 54.
 Ahmed Abdul Zaher aliingiza bao la pili kwa Ahly katika dakika 78.
Hata hivyo mabingwa wa Misri walipungua kwa mtu mmoja na kusalia 10 dakika sita baada ya mlinzi Sherif Abdel Fadil kuondolewa uwanjani kwa kumfanyia vibaya Daine Klate.
Pirates, ambao walichukua taji mwaka 1995, walicheza kadri ya uwezo wao, lakini waliondokewa na matumaini pale Ahly walipoingiza bao lao la pili katika uwanja uliokuwa umesongamano wa watu mjini Cairo.
Hata hivyo mabingwa hao wa Afrika Kusini walikosa nafasi kadhaa za kuingiza bao.
Ahly wamepata kombe hilo pamoja na kitita cha dola milioni moja na nusu
Pia watawakilisha Afrika katika kombe la dunia la klabu bingwa duniani litakalofanyika nchini Morocco mwezi ujao.
Mamia ya mashabiki wa Ahly walikabiliana na polisi kabla ya mechi hiyo kuanza. 
Ni mechi ya kwanza kubwa ambako mashabiki wameruhusiwa kuingia uwanjani tangu watu 74 wengi waliokuwa mashabiki wa Al Ahly , waliuawa katika mechi iliyokumbwa na vurugu mwaka jana.
Polisi wlailazimika kutumia gesi ya kutoa machozi, kuwatawanya mashabiki waliokuwa wanatupia mawe huku wakiingia kwa lazima ndani ya uwanja.

No comments:

Post a Comment