KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 11, 2013

KATIBU WA FIFA KUWATOA HOFU GHANA KUHUSU CAIRO

Katibu mkuu wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Jerome Valcke anakutana na waziri wa michezo wa Ghana pamoja na maafisa wengine nchini Togo leo kuwahakikishia mipango wa usalama kwa ajili ya mchezo wa mtoano katika kinyang'anyiro cha kuwania tikiti ya kucheza katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil mchezo ambao utafanyika mjini Cairo wiki ijayo.
Ghana ilisema kuwa inahofia usalama nchini Misri baada ya mara kwa mara nchi hiyo kukumbwa na maandamano na huenda mashabiki wa Misri wakafanya maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi nchini humo katika uwanja wa mjini Cairo wa Juni 30 ambao unamilikiwa na jeshi.

No comments:

Post a Comment