KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 11, 2013

MAKOCHA WA LIGI YA ENGLAND WANASEMA NINI BAADA YA MATOKEO YA MWISHO WA WIKI?

Kocha wa Manchester United David Moyes ameonya kuwa timu yake bado inapaswa kupiga hatua zaidi baada ya kupata uhai kidogo katika kinyang'anyiro cha kuwania kutetea ubingwa wake wa ligi ya Uingereza Premier League, kwa kuishinda Arsenal jijini London hapo jana ambao wanaongoza ligi hiyo kwa sasa.

Moyes ameshuhudia timu yake ikipata kipigo dhidi ya Liverpool, mahasimu wao wakubwa Manchester City, na hata West Bromwich Albion tangu mwanzoni mwa msimu, lakini ushindi wa bao 1-0 jana Jumapili dhidi ya Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford umeiweka points tano tu nyuma ya Arsenal.
Kipigo dhidi ya Man City na Tottenham Hotspurs mwishoni mwa juma , pamoja na sare ya Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion, vimesaidia Manchester United kujiweka miongoni mwa timu zinazowania ubingwa , lakini Moyes amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya.
"Itachukua muda kidogo kwangu mimi kuweka kila kitu katika mtazamo ninaoutaka".
Manuel Pellegrini kocha wa Man City amesema kikosi chake kinapaswa kucheza vizuri zaidi ugenini iwapo kitawania nafasi ya kushinda ubingwa wa Premier League msimu huu.
Kikosi cha Pellegrini kina rekodi safi sana nyumbani kikishinda michezo mitano katika ligi hadi sasa msimu huu, lakini ugenini kimevurunda.
Licha ya kupata ushindi hivi karibuni ugenini katika Champions League na kombe la ligi, City wamepata points nne tu katika jumla ya points 18 uginini katika ligi ya Uingereza baada ya kupata kipigo cha nne kwa bao moja bila majibu dhidi ya Sunderland jana Jumapili.

No comments:

Post a Comment