KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 9, 2013

Marcelo Lippi ameweka historia

Marcelo Lippi ameweka historia kufuatia klabu yake ya Guangzhou Evergrande kutwaa taji la AFC Champions League baada ya kupata faida ya goli la ugenini baada ya kumaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Seoul mchezo uliopigwa katika uwanja wa Tianhe hapo jana Jumamosi.
Sare hiyo ilitosha kukipa kikosi cha Lippi taji baada ya sare nyingine ya mchezo wa kwanza ya bao 2-2 huku mabingwa hao wa Chinese Super League wakikamilisha mataji mawili ya ligi ya nyumbani na bara la Asia. 
Evergrande pia imekuwa timu ya kwanza kutoka nchini Chinese kutwaa taji barani Asia kwa kipindi cha miaka 23 na ya kwanza kutwaa taji la soka nchini China chini ya mfumo mpya wa uendeshaji wa ligi huku Lippi akiwa kocha wa kwanza kutwaa Champions Leagues kote Ulaya na Asia pamoja na dunia.