KLABU KIGOGO ya nchini Ethiopia St. George amemtupia virago mshambuliaji nyota wa zamani Azam fc ya Tanzania Mganda Robert Ssentongo ikiwa ni miezi michache tu tangu ajiunge nayo akitokea klabu ya URA(Uganda Revenue Authority).
Mshambuliaji huyo ambaye aliingia kandarasi ya kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili mwezi Januari mwaka huu ameshindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kitu ambacho afisa wa klabu hiyo Ephraim Gezachew amesema ni kutokana na kushindwa kujituma.
Amenukuliwa afisa huyo kupitia mtandao wa mtnfootball.com akisema
“Kama kuna klabu yoyote itamchukua tuko tayari kumuachia aende kwa barua”.
“He said a two year contract with us but we are ready to let him go”, he added.
Gezachew akaendelea mbali kwa kusema wamesikitishwa na Ssentongo kwasababu wametumia pesa nyingi kumsajili lakini kile alichokizalisha kimekuwa kidogo mno.
Katika hatua nyingine, Ssentongo ameripotiwa akilalamika kuwa amerejea Uganda kwakuwa klabu ya St. George haijamlipa mshahara wake wa miezi miwili, malalamiko ambayo yamepuuzwa kwani wenzie akina Robert
Odongkara na Isaac Isinde hajalalamikia hilo.
Ssentongo ameungana na waganda wenzake walioshindwa kufanya vema katika soka la kulipwa kama Emmanuel Okwi, Godfrey Walusimbi, Vincent Kayizzi, Mike Mutyaba, Moses Oloya, Geoffrey ‘Baba’ Kizito na Geoffrey Sserunkuma ambao wote kwa pamoja tayari wamesha rudi nchini Uganda.

No comments:
Post a Comment