Mshambuliaji mkongwe wa zamani wa Arsenal Thierry Henry hii leo ameonekana akifanya mazoezi na klabu yake hiyo ya zamani wakati huu ambapo Arsenal inajiaandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Southampton Jumamosi.
Mshambuliaji huyo kwasasa yuko katika mapumziko ya ligi ya Marekani MLS ya majira ya baridi akiwa bado na klabu yake ya New York Red Bulls na kwa wiki kadhaa sasa akiwa mapumzikoni.
Henry
aliichezea kwa miaka minae Arsenal, ambapo pia aliifungia jumla ya mabao 226 katika mashindano yote.
Aliwahi kurejea kwa mkopo katika msimu wa 2011/12ambapo alifanikiwa kufunga goli moja tu.
Henry alionekana mwenye tabasamu kuchezka na kutania muda wote wakati wa mazoezi.
Henry akiwa na Laurent Koscielny, Nacho Montreal na Olivier Giroud.
Arsenal wanatarajiwa kuwa na mshambuliaji wao aliyerejea kutoka katika majeraha Theo Walcott ambaye alikosekana kwa kipindi cha takribani miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Mlinzi wa kimataifa wa Ujerumani Per Mertesacker, ambaye alifunga goli uwanja wa Wembley Jumanne amepona baada ya kuwa nje katika mchezo waliopokea kichapo kutoka kwa Manchester
United, lakini kiungo Mathieu Flamini atakosekana akitumikia adahabu.
Kiungo wa kimataifa wa England Jack Wilshere amerejea baada ya majukumu ya kimataifa lakini akiwa hayuko sawa.
Yaya Sanogo (mgongo), Lukas Podolski (msuli),
Alex Oxlade-Chamberlain na Abou Diaby (wote miguu) wote watakuwa nje.
Hapa akiwa na Emmanuel Frimpong
No comments:
Post a Comment