Mbio za New York City Marathon zilirejea tena baada ya kukosekana kwa
mwaka mmoja, huku kukiwa na umati mkubwa wa mashabiki, na kiwango
kikubwa cha usalama, pamoja na bingwa ambaye anafahamika vyema.
Geoffrey Mutai alifanikiwa kulitetea taji lake hapo jana, wakati mkenya
mwenzake Priscah Jeptoo akitoka nyuma na kushinda taji la wanawake.
Buzunesh Deba alimaliza katika nafasi ya pili kwa mara ya pili
mfululizo.
Mashabiki walisahau matukio ya mwaka jana, ambapo mbio za marathon za
NYC zilifutwa kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa kimbunga Sandy.
Na baada
ya milipuko ya mabomu iliyozikumba mbio za marathon za Boston mwezi
Aprili, hali ya usalama iliimarishwa kabisa katika jiji la New York
kulikoandaliwa mbio hizo.
Mutai alitumia muda wa 2:08:24 mbele ya
nambari mbili Tsegaye Kebede wa Ethiopia.
April wa Afrika Kusini
alichukua nafasi ya tatu.

No comments:
Post a Comment