 Uganda Cranes imekuwa ni timu ya pili kupata nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la chalenji baada ya Sudan katika michuano ya GOtv CECAFA Senior Challenge Cup inayoendelea nchini Kenya.
 Uganda Cranes imekuwa ni timu ya pili kupata nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la chalenji baada ya Sudan katika michuano ya GOtv CECAFA Senior Challenge Cup inayoendelea nchini Kenya. 
The Crane imetinga hatua hiyo muhimu kufuatia mabingwa hao mara 13 wa CECAFA
kuwashinda Eritrea kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa ndani ya uwanja wa nyasi bandia wa City Stadium, ulioko jijini Nairobi. 
Mpaka kufiakia mapumziko mshambuliaji wa zamani wa Simba SC Emma Okwi ambaye alikosekana katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Rwanda ijumaa iliyopita uwanja wa Nyayo alikuwa tayari amekwisha kuifungia Uganda mabao yote mawili.
Mabao yote hayo aliyafunga kutokana na jitihada kubwa za msahambuliaji wa Dan ‘Muzei’ Sserunkuma .
Bao la tatu liliwekwa wavuni na mshambuliaji wa Yanga ya Tanzania Diego 
Hamis Kizza kwa njia ya penati ikiwa ni baada ya  
Sserukuma kuangushwa katika eneo la hatari na mlinzi wa Eritrea Suarfael 
Tesfamekal ambaye pia alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi kutoka nchini Burundi Thiery Nkurunziza. 
Kesho itakuwa ni zamu ya Zanziba dhidi ya Kenya huku mchezo mwingine ukiwa ni baina ya Sudani Kusini dhidi ya Ethiopia. Michezo yote itachezewa katika mji wa Nakuru.
Team Line-Ups: 
UGANDA: Benjamin Ochan, Nicholas Wadada, 
Godfrey Walusimbi, Savio Kabugo, Richard Kassaa, Khalid Aucho, Baaba 
Kizito (’87 Joseph Mpande), Diego Kizza (’62 Isaac Muleme), Dan 
Sserunkuuma, Brian Majwega (’47 Said Kyeyune), Emma Okwi 
ERITREA: Abdulahi Abdurahman (GK), Haile 
Goitom , Yasser Omer ,Yonas Selemun, Suarfael Tesfamekal , Samson 
Estifanos , Yekalo Gezae , Yonathan Selemon , Muner Ahmed , Haben Berhan
 (’61 Omer Selahaden) , Serak Beyene. 
Officials:
Center Referee: Thiery Nkurunizza (Burundi),
 1st Assistant:Zakara Fraser (South Sudan), Gilbert Cheruiyot (Rwanda), 
4th Official: Ferej Tamim (Zanizbar)
Referees Inspector: Ali Ahmed (Somalia)
Media Officers: Rogers Mulindwa (Uganda) and Badri Bakheit (Sudan)
 

No comments:
Post a Comment