KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 1, 2013

CECAFA CHALENJI CUP:Leo ni The Kilimanjaro Stars dhidi ya Somalia waliokula 7-0 Kampala 2012

Kikosi cha Kikimanjaro Stars
Kocha mkuu kikosi cha Kilimajaro stars Kim Poulsen anaamini kikosi chake kinauwezo wa kuifunga Somalia katika mchezo wa leo jioni ya leo wa kundi B la michuano ya GOtv Cecafa Cup 2013 mchezo ambao utapigwa katika dimba la Nyayo hii leo.

The Kilimanjaro stars ilianza kampeni ya michuano hiyo kwa kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa Afrika mwaka 2012 Zambia maarufu kama Chipolopolo lakini kocha Mdenish Kim anadhani kuwa mchezo huo dhidi ya Somalia maarufu kama Ocean Stars unaweza kuwa mgumu.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja Machakos uliathiriwa na pichi mbovu ambayo ililalamikiwa na kocha Kim, lakini mara hii mchezo utakuwa ukichezwa Uwanja wa Nyayo ambao una ubora katika sehemu yake ya kuchezea.
 
“Nategemea mchezo mzuri kwa kikosi changu mara hii”
“Dhidi ya Zambia tulicheza vizuri lakini tuliathiriwa na uwanja mbovu haukuruhusu kasi yetu, lakini nikuambie tu tutawashinda Somalia”.
Kim Poulsen kwa mara nyingine tena atawakosa washambuliaji wake wawili wanaochezea TP Mazembe ya DRC Congo Mbwana Ally Samata na Tahomas Ulimwengu ambao jana walikuwa wanamalizia majukumu yao katika klabu hiyo katika michuano ya vilabu ya shirikisho dhidi ya CS Sfaxien ya Tanisia na wakitarajiwa kuelekea Nairobi moja kwa moja.

“Tuliwakosa katika mchezo dhidi ya Zambia na tutawakosa katika mchezo wa leo dhidi ya Somalia lakini nawaamini wachezaji wangu waliopo”.

Kukosekana kwa washambuliaji hao kunatoa nafasi kwa Kim kuwatumia Mrisho Alfan Ngassa, Amri Kiemba na Salum Abubaker “Sure Boy”.
Kiungo mzoefu wa Yanga FC Athman Iddi 'Chuji' leo anatazamiwa kuanza katika kikosi cha kwanza tofauti na mchezo uliopita ambao aliingia akitokea benchi.

Somalia ambao walipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Burundi kwa kufungwa 2-0 watalazimika kushinda ili kurudisha matumaini angalau ya kutinga robo fainali.

Mara ya mwisho pande hizo mbili kukutana ilikuwa ni katika michuano ya Chalenji iliyofanyika Uganda mwaka 2012 ambapo Kilimanjaro Stars iliivuruga Somalia kwa kuwapa kichapo cha mbwa mwizi cha mabao 7-0 mchezo uliopigwa uwanja wa Lugogo jijini Kampala.
Mrisho Ngasa na John Boko walioisambaratisha Somalia Chalenji ya Uganda, Ngasa alifunga mabao 5 na Boko mabao 2.

Katika mchezo wa mwaka jana mabao ya Kilimanjaro yaliwekwa wavuni na Mrisho Ngasa aliyefunga mabao 5 na John Boko 'Adebayor' aliyefunga mabao 2.