Jose Mourinho amemfagilia Ashley Cole kuwa ni model professional na anategemea kuendelea kupata huduma yake kwa muda mrefu ndani ya Chelesea kwa kumpatia mkataba mpya.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa kushoto wa England ataanza katika mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest katika dimba la Stamford Bridge ukiwa ni mchezo wa kundi E kwa mara ya kwanza kufuatia kukosekana kwa takribani mwezi mzima.
Cole ambaye anaelekea kufikisha umri wa miaka 33 wiki ijayo amekuwa katika benchi au kucheza akitokea Benchi ambapo Mourinho amekuwa akimuanzisha Cesar Azpilicueta kushoto.
Mkataba wa mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal unatarajiwa kumalizaka mwishoni mwa msimu lakini Mourinho hana wasiwasi kuwa kuwa Cole bada ana nafasi ya kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo siku za usoni.
Amekaririwa akisema
"namjua vema ni rahisi kudhani kuwa hana raha na hali ilivyo sasa ndani ya klabu lakini jinsi anavyofanya mazoezi na tabia yake kwa kweli ni 'super professional'.

No comments:
Post a Comment