Klabu ya Ac Milan imemfuta kazi Massimiliano Allegri na kumpandisha
ngazi Mauro Tassotti kama kocha wa muda, baada ya vigogo hao wa soka
Italia kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika Serie A
Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya vigogo hao wa soka kuabishwa kwa
kupewa kichapo cha mabao 4-3 na klabu iliyopandishwa ngazi
msimu huu Sassulo.
Huku wakiwa katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa ligi kuu ya
Italia Serie A, Milan wametangaza uamuzi huo kupitia tovuti yao.
Wameshinda mechi 19 pekee msimu huu na Allegry alikuwa tayari ametangaza
katika kipindi kifupi cha mapumziko ya majira ya baridi kuwa huenda
akaondoka mwishoni mwa msimu.
Allegri alichukua usukani mnamo mwaka wa 2010 na akashinda
Serie A katika msimu wake wa kwanza kisha akamaliza katika nafasi za
pili na tatu katika misimu iliyofuata. Hata hivyo, AC Milan ndio timu
pekee ya Italia kufuzu kazika awamu ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
na watapambana na Atletico Madrid mwezi ujao.
Kwingineko, barani Ulaya, Real Madrid waliitumia faida ya mchuano
uliotoka sare kati ya viongozi wa La liga Atletico Madrid na Barcelona
kwa kusajili ushindi wa goli moja kwa sifuri nyumbani kwa Espanyol na
kupunguza pengo baina ya viongozi hao hadi pointi tatu pekee..wakati
ikiwa imefikia nusu ya msimu. Bao la kichwa alililofunga Pepe lilitosha
kuwapa Madrid pointi tatu na sasa wako katika nafasi ya tatu na pointi
47.
Kule England, Manchester City walisonga hali kileleni mwa Premier
League, baada ya kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya
Newcastle baada ya Chelsea kushikilia usukani kwa siku moja kufuatia
ushindi wao wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Hull.
Arsenal waliteremka hadi nafasi ya tatu lakini leo wanaweza tena kurejea
kileleni, kama watawashinda Aston Villa. Kwingineko magoli yalizidi
kutiririka kwa upande wa Liverpool ambao wako katika nafasi ya nne,
baada ya Luis Suarez kufunga mawili katika ushindi wao wa magoli matano
kwa matatu dhidi ya Stoke.
No comments:
Post a Comment