Nyota kinda wa Uganda Cranes Junior Yunus Sentamu, amesema ana njaa ya kukiongoza kikosi cha timu yake ya taifa kufikia katika hatua ya pili ya mashindano ya wachezaji wa ndani ya soka barani Afrika 2014 CHAN.
Kinda huyo mwenyen umri wa miaka 19 ambaye alikuwepo katika mchezo wa kwanza wa fainali za mataiafa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN ambapo alifanikiwa kuandika bao la pili na kuwanyamazisha Burkina Faso kwa ushindi wa mabao 2-1 mchezo wa kundi B uliopigwa Athlone Stadium jana Jumapili.
“nina furaha nimefunga magoli mawili na kuwa mchezaji bora wa mchezo huo .Nitafanya kazi kubwa na kujituma zaidi kuisaidia timu yangu kuingia katika hatua ya pili ya mshindano” amekaririwa mshambuliaji huyo mwenye aibu wa SC Vipers.
Kocha wa Cranes Milutin ‘Micho’ alimpongeza sana Sentamu ambaye amemtabiria kuwa ni nyota wa baadaye wa kujivunia wa soka la Uganda.
Sentau ameipeleka tunzo yake ya kwanza ya mchezaji wa mchezo yaani 'man of the game' kwa familia yake ambayo amesema imekuwa ikimuunga sana mkono katika kazi yake ya soka.
No comments:
Post a Comment