Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
Enzi
zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338
ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa
timu hiyo.
Alianza
vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la
Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza
mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza
kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Aprili
mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya
kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake,
John Metgod.
Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
Baada
ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda
kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja.
Ajax
ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka
1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya
Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana,
ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
Mwaka
2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na
kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba
tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati
ya 21.
No comments:
Post a Comment