KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Manchester City: Sergio Aguero atarejea kikosini kesho kuwakamua Blackburn FA Cup.

Sergio Aguero atarejea katika kikosi cha Manchester City hapo kesho ambapo kikosi hicho kitakuwa na mchezo wa roundi ya tatu mchezo wa marudiano wa michuano ya FA dhidi ya Blackburn katika dimba la Etihad Stadium.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa nje ya uwanja tangu Disemba 14 kufuatia kusumbuliwa na msuli maumivu aliyoyapata katika mchezo wa ushindi mnene wa mabao 6-3 dhidi ya Arsenal.
Anakaririwa meneja wa City Manuel Pellegrini akisema kuwa 
"Sergio anafanya kazi sasa na kikosi kizima na yuko katika orodha ya wachezaji wangu kuelekea katika mchezo wa kesho dhidi ya Blackburn".
Aguero ndio mfungaji anayeongoza kwa ufungaji katika kikosi cha City akiwa tayari amefunga jumla ya magoli 19 msimu huu.

City imeshinda michezo nane tangu kuumia kwa Aguero ikiwa ni pamoja na kwenda sare ya bai 1-1 dhidi ya Blackburn katika mchezo kwanza lakini Pellegrini anadhani mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ni sehemu muhimu sana katika kikosi chake.
"Ni muhimu katika kikosi chetu," amekaririwa meneja huyo wa zamani wa Malaga akisema
 "Haijalishi pamoja na kufunga magoli mengi akiwa hayupo,  Sergio ataendelea kuwa muhimu na tunafuraha amerejea" 

Kikosi cha kwanza kabla ya kesho ni 'provisional squad: Hart, Pantilimon, Zabaleta, Richards, Kompany, Lescott, Nastasic, Demichelis, Boyata, Kolarov, Clichy, Milner, Navas, Fernandinho, Garcia, Negredo, Dzeko, Lopes, Aguero.

No comments:

Post a Comment