KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 31, 2014

Usajili januari: Chelsea yamsajili kwa muda mfupi na kumkabidhi kwa mkopo mlinzi Kurt Zouma kwa St Etienne

Difenda wa Ufaransa wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Kurt Zouma hii leo amekua gumzo kubwa katika harakati za kuwahi muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili ambapo ndani ya masaa kadhaa hii leo amefanikiwa kujiunga na Chelsea akitokea St Etienne na punde tu akakabidhiwa akakabidhiwa tena kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama 'Ligue 1' kwa mkopo katika kipindi kilichosalia cha msimu.
Taarifa hizi zimethibitishwa na klabu hiyo ya London.

Zouma mwenye umri wa miaka 19, alijiunga na akademi ya St Etienne akiwa na miaka 14, na akawa mchezaji mtaalamu mwaka 2011 na anaonekana kama uwekezaji wa muda mrefu wa Chelsea huku nahodha John Terry, 33, akikaribia mwisho wa uchezaji wake katika klabu hiyo.

Chelsea wamethibitisha kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo wa (www.chelseafc.com) kwamba walikuwa wamepata saini yake kwa mkataba wa miaka mitano na nusu. 

Zouma ameichezea St Etienne michezo 52 katika ligi, michezo 12 msimu huu, lakini alipigwa marufuku ya mechi 10 kwa kumchezea visivyo mchezaji wa Sochaux Thomas Guerbert na kumvunja mguu pamoja na kutegua kifundo chake cha mguu.

Mchezaji thabiti, Zouma alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda taji la dunia la U-20 kipindi kilichopita cha majira ya joto na aliitwa na kocha Didier Deschamps kabla ya mechi ya kirafiki ya Oktoba dhidi ya Australia ingawa hakucheza
.
Ripoti kwenye vyombo vya habari vilisema alinunuliwa takriban pauni 12.5 milioni ($20.62 milioni) na ndiye mchezaji wa tatu mkuu kujiunga na Chelsea kipindi cha kuhama wachezaji cha Januari.
Nemanja Matic alijiunga nao kutoka Benfica na Mohamed Salah kutoka Basle huku Kevin de Bruyne na Juan Mata wakihama klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment