KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 31, 2014

Uwanja wa Chamazi waruhusiwa na FIFA kuandaa michezo ya kimataifa unakuwa uwanja wa kwanza Afrika mashariki

Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanza unaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki  kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu

Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF “ku-host” mashindano yakimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “ku-host” mech za CAF

Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripotiCAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechizinazoandaliwa na CAF

Uongozi wa Azam FC unatoa shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais JamalMalinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazina uweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.

Azam FC ingependa kuwataarifu wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za  CAF zitachezwa AzamComplex Chamazi

Unaweza kuuangalia uwanja huu kwa ku-bofya hapa

No comments:

Post a Comment