Washabiki
wa mpira wa miguu nchini watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa
miguu ya wanawake (Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC)
itachezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga
Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka
huu kwa mabao 2-1 iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake
Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi
(Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi
wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis
Iratunga kutoka Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa
(Februari 26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye
atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways.
YANGA, SIMBA
ZAINGIZA MIL 100/- VPL
Mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizohusisha timu za Yanga na Simba, na kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zimeingiza jumla ya sh.
101,165,000.
Yanga
ambayo iibugiza Ruvu Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza sh. 68,450,000
kutokana na washabiki 11,972 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh.
20,000.
Katika
mechi hiyo kila klabu ilipata mgao wa sh. 15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 10,441,525.42. Gharama
za tiketi ni sh. 3,813,600 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata sh.
4,877,538.71. Uwanja sh. 8,129,231.19.
Gharama
za mchezo zilikuwa sh. 4,877,538.71 wakati Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 2,438,769.36. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata sh.
945,110.
Nayo
mechi ya Simba na JKT Ruvu ilishuhudia na watazamaji 5,850 na kuingiza sh.
32,715,00 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 4,990,423.73.
Kila
klabu ilipata mgawo wa sh. 7,428,742 wakati tiketi ni sh. 2,542,400 huku
gharama za mechi zikiwa 2,266,395.86. Uwanja ulipata sh. 3,777,326.44 wakati
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni sh. 2,266,395.86.
Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulipata mgawo wa sh. 1,133,167.93 na Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 881,376.17.
RWIZA
KUSIMAMIA MECHI YA TP MAZEMBE
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza Kishongole kuwa Kamishna
wa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya TP Mazembe na Asres De
Douala ya Cameroon.
Mechi
hiyo ya hatua ya 16 itafanyika kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu jijini
Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kuchezeshwa na waamuzi
kutoka Uganda.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Denis Batte wakati wasaidizi wake ni Mark Ssonko, Samuel
Kayondo na Mashood Ssali.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment