Mashabiki wa Coastal Union wakishangilia baada ya kuingia bao la pili dakika chache kabla ya mpira kumalizika. |
Ally Nassor 'Ufudu' akitumia mbinu za kumkinga golikipa wa Mbeya City
katika moja ya kona zilizopigwa kwenye mchezo wa leo uliomalizka kwa Coatal kupata mabao 2-0.
Danny Lyanga wa Coastal kulia akikokota mpira huku mchezai wa Mbeya City akitafuta mbinu za kumdhibiti.
Kocha wa Coastal Union Yusuf Chipo akiwahimiza wachezaji wake wapande juu wasikabe.
Haruna Moshi 'Boban', akifanya vitu vyake uwanjani leo kuwaonyesha vijana kwamba bado yumo.
Winga wa Coastal Union Danny Lyanga akiambaa na mpira huku akitafuta mbinu za kupiga krosi.
Mlinzi wa pembeni Coastal Union, Abdi Banda akimiliki mpira bila ya wasiwasi wowote.
Mohammed Miraji 'aliebebwa' akishangilia bao la kwanza mnamo dakika ya 79 kipindi cha pili.
Mashabiki wa Mbeya City wakiwa hawaamini wanachokiona namna vijana wa Chipo walivyofanya mambo.
Mshabiki wa Coastal Union wakishangilia timu yao katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ngumu ya Mbeya City ya Mbeya. |
Kutoka kushoto Juma Nyoso, Mohammed Miraji na Kenneth masumbuko wakishangilia bao la pili lililofungwa na Moammed Miraji.
Mbeya City kawaida yao hufanya mazoezi baada ya mechi, lakini Mkwakwani walifanya kidogo na kuacha.
Mashabiki wa Coastal Union wakishangilia baada ya mechi.
HATIMAE historia imeandikwa kwatika jiji la Tanga baada ya
Coastal Union ‘Wagosi wa kaya’ kuwa timu ya pili kuifunga Mbeya City katika Ligi
Kuu, lakini vilevile ni ya kwanza kuifunga mabao mengi.
Bao la kwanza liliingizwa kimiani mnamo dakika ya 79 baada
ya Mohammed Miraji, kuunganisha pasi ya Danny Lyanga ambae alipokea mpira
uliorushwa na Abdi Banda.
Mohammed, aliruka juu na mchezaji wa Mbeya City akapiga
kichwa kilichopaa na kurudi langoni kama masihara ukisindikizwa na beki wa
Mbeya City. Baada ya bao hilo Coastal Union waliendelea kulisakama lango la
Mbeya City kwa takriban dakika tano.
Aidha bao la pili lilikuwa juhudi binafsi za mchezaji
chipukizi Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’ ambapo alipokea pasi nyuma kidogo ya
18, akamzidi nguvu kiungo wa Mbeya City akapiga chenga mbili na kuinua macho
kumtazama Burhani, golikipa wa Mbeya City. Akakunjuka shuti kali kwa mguu wa
kulia lililomzidi nguvu Burhani na kuandika bao la pili dakika mbili kabla ya
mwamuzi wa leo Zacharia Jacob, kutoka Pwani kumaliza mchezo.
Hata hivyo Wagosi wa Kaya walinza mpira wa leo kwa kusuasua
ambapo kipindi cha kwanza walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuambulia
kitu. Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika Wagosi walicheza chini ya kiwango
hali iliyowanyima raha mashabiki wa Wagosi huku ikiwaamsha mashabiki wachache
wa Mbeya City waliosafiri na timu kutoka jijini Mbeya.
Kocha wa Wagosi Yusuf Chipo, alifanya mabadiliko kwa kuwatoa
Ally Nassor ‘Ufudu’ akaingia Kenneth masumbuko, baadae akamtoa Ayoub Semstawa
akaingia Yayo kato halafu akakamilisha mabadiliko ya leo kwa kumtoa Crispian
Odula na kumuingiza Mohammed Miraji ambae alikuwa mfalme wa echi ya leo.
Mabadiliko hayo yalileta uhai kwa timu hasa winga Masumbuko
alipoingiza mipira mingi lakini Yayo kato na Haruna Moshi ‘Boban’ walishindwa
kuzitendea haki krosi za winga huyo msumbufu.
Katika hatua nyingine Mbeya City, walifanya mashambulizi
mengi katika lango la Wagosi lakini uimara wa mabeki Abdi banda, Nyoso, Kibacha
na Chuma ulimsaidia golikipa Shaaban Kado kupata muda mzuri wa kudaka kwa
kujiamini.
Kutokana na matokeo hayo Coastal Union wamepaa mpaka nafasi
ya tano wakitoka nafasi ya saba huku wakijizolea point 25. Kupaa huko
kumetokana na Ruvu Shooting waliokuwa nafasi ya tano kuchapwa mabao 7-0 na
Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment