KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 17, 2014

Nani kurithi nafasi ya unahodha Old Trafford baada ya Vidic? hii hapa ni orodha rasmi fupi ya United.

Hatma ya baadaye ya Robin van Persie ndani ya Manchester United inaendelea kuonekana kuwa katika hali ya wasiwasi ilhali wiki za hivi karibuni kuna dalili za mshambliaji huyo kuchukua nafasi ya Nemanja Vidic katika nafasi ya unahodha.
 
Mshambuliaji huyo mduchi ambaye kwasasa ni skipper katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi amekuwa katika orodha ya watu wa mbele kuchukua nafasi ya kitambaa cha unahodha kuanzia msimu ujao baada ya kuthibitika kuwa Vidic ataondoka katika klabu hiyo wakati wa kiangazi.
Hata hivyo tayari mtandao wa United umeorodhesha majina matano ambayo yanaweza kuchukua unahodha ambapo jina la Van Persie halipo.
Katika orodha hiyo lipo jina la Wayne Rooney ambaye anatarajiwa kuongeza muda wa kuichezea klabu hiyo sambamba na majina ya David De Gea, Jonny Evans, Phil Jones na Darren Fletcher.
Van Persie bado anayo nafasi bado ya kupata nafasi hiyo kwani inakumbukwa mwaka uliopita aliwahi kuwa nahodha katika kikosi cha Arsenal, ilhali pia inakumbukwa alikua nahodha katika safari ya United katika ziara ta mashariki ya mbali wakati wa kiangazi.
Bado kumekuwepo na taarifa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hajatulia ndani ya Old Trafford iliyochini ya meneja David Moyes. Alikuwa benchi katika kipindi cha wiki sita kutoka na kuwa majeruhi katika kipindi cha mwezi Disemba kuelekea mwaka mpya na anaendelea kupigania kiwango kurejesha kiwango cha msimu uliopita.
Patrice Evra, pia hayupo katika orodha hiyo na anaweza akaondoka ndani ya klabu hiyo kama ilivyo kwa Vidic baada ya kumalizika msimu.
Shortlist: United's official website assesses five potential candidates
Orodha fupi ya majina kupitia mtandao wa United kama inavyoonekana


Food for thought: Vidic has confirmed he is leaving the club in the summer while Van Persie's future has also been the subject of much speculation
Vidic kushoto juu amethibisha kuondoka United kiangazi huku hatma ya Van Persie pichani juu kulia ikiwa bado tete.


Favourite: Wayne Rooney is the bookmakers' choice to wear the armband from next season

No comments:

Post a Comment